Monday, June 18, 2012
maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika jijini Mwanza leo ~ MTAA KWA MTAA
TAARIFA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
YALIYOFANYIKA KIMKOA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA 16/6/2011
1.0 Utangulizi
Siku ya siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa tarehe 16, Juni ya kila mwaka.
Siku hii inaadhimishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa
Nchi huru za Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya kinyama
waliofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mnamo
mwaka 1976. Hapa nchini kuna utaratibu wa kuazimisha Kitaifa kila baada ya
miaka mitano, mwaka huu maadhimisho yamefanyika Kimkoa. Kwa Mkoa wa Dar
es Salaam maadhimisho haya yalifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Hii ni kutokana na utaratibu tuliojiwekea wa
kuadhimisha kwa kila mwaka kwa awamu katika Halmashauri za Manispaa za
Mkoa wa Dar es salaam.
2.0 Lengo la Maadhimisho
Siku hii huadhimishwa kwa lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa
watoto nchini Afrika ya Kusini wakati wakidai haki zao za msingi, pia
kuwakumbusha wazazi/walezi na jamii kwa ujumla juu ya haki na wajibu wa
jamii katika kuwalea watoto. Aidha, hutoa nafasi ya kuwakumbusha watoto haki
na wajibu wao kama watoto katika Taifa.
3.0 Kauli mbiu
Kauli mbiu ya mwaka huu (2011) inasema “Tuungane Pamoja Kuchukua
Hatua za Haraka Kushughulikia Tatizo la Watoto Wanaoishi Mitaani”.
Ikiwa na maana ya kukumbusha umuhimu wa wazazi, walezi wadau wote katika
kushughulikia tatizo la watoto wanaoishi mitaani na kwamba watoto hawa ni
wetu na ndio msingi mkubwa wa kuleta maendeleo ya nchi hii kwa siku za
baadae. Hivyo basi, jamii tunao wajibu kipekee wa kumuandaa mtoto wa taifa
hili ili awe raia mwema.
4.0 Yaliyojitokeza
• Risala ya watoto
• Hotuba ya Mgeni rasmi
• Vikundi vya burudani
• Mgeni rasmi kutembelea mabanda
4.1 Risala ya watoto
Watoto walipata nafasi ya kusoma risala mbele ya Mgeni rasmi, wazazi, walezi na
wadau mbalimbali ambayo iliwasilishwa kwa niaba ya watoto wenzao wa Mkoa
wa Dar es salaam. Katika risala yao watoto walimshukuru mgeni rasmi kwa
kukubali kuungana nao katika maadhimisho hayo. Risala hiyo ilitoa ujumbe
mbalimbali ikiwa ni pamoja na;-
Jamii kuweka utaratibu wa kuwahudumia watoto wote bila kubagua
•
Serikali iangalie namna ya kuondoa umaskini wa kipato katika ngazi ya
•
familia
Baadhi ya watu katika jamii waache tamaa ya kuchukua mali na kuwaacha
•
watoto wakihangaika mitaani pindi wazazi wao wanapofariki dunia.
Pia, risala ilibainisha vyanzo vya watoto kwenda kuishi mitaani kama vile,
kutopata upendo kutoka kwa wazazi na walezi, matatizo mimba za utotoni, utoro
shuleni na tamaa. Hivyo jamii na watoto wanapaswa wafahamu haki na wajibu
wao.
4.2 Hotuba ya Mgeni rasmi
Hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck
Sadick katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ilisomwa na Ndugu E.
Ntandu Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Mipango na Uratibu aliyemwakilisha
Kaimu Mkuu wa Mkoa katika maadhimisho hayo. Katika hotuba yake Mgeni rasmi
aliwashukuru Wataalamu wa Sekretarieti na Halmashauri za Manispaa katika
kuandaa siku hiyo. Aidha, alitoa Shukrani za dhati kwa Shirika la AMREF, Benki
ya CRDB, Benki ya Wananchi, Shirika lisilo la kiserikali la Dar Urban Plan na
Wadau wengine wote kwa kutambua mchango wao katika kuadhimisha siku ya
Mtoto wa Afrika ndani ya Mkoa wetu. Pia alisisitiza kwamba kwa mwaka ujao
wazazi na walezi wengi wahamasishwe ili waungane pamoja na watoto wao
katika kuadhimisha siku hiyo ili ujumbe unapotolewa uweze kuwafikia.
Mgeni rasmi alitoa wito kwa jamii itimize wajibu wake kama kauli mbiu ya
mwaka huu unavyotutaka na kuahidi kwamba Mkoa utaendelea kutoa fursa kwa
watoto ili kuweza kutoa maoni yao kwa Maendeleo ya Taifa na kuwachukua
hatua kali za kisheria wale wote wanaoendeleza ukatili dhidi ya watoto.
Vikundi vya burudani.
4.3
Watoto walipata nafasi ya kuonesha burudani mbalimbali kwa Mgeni rasmi na
watu wote waliofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Burudani hizo zilikuwa ni
pamoja na Ngoma ya mganda, kwaya na maigizo zikiwa zimebeba ujumbe
mbalimbali kama vile, ajira za watoto zikomeshwe na wazazi na walezi
wapelekwe watoto shuleni kwani uridhi pekee wa wazazi kwa watoto ni elimu,
jamii iwalee na kuwatunza watoto. Aidha, Serikali iendelee kutoa elimu kwa jamii
juu ya haki na wajibu wa watoto na jamii.
4.4 Mgeni rasmi kutembelea mabanda
Mgeni rasmi alipata nafasi ya kutembelea mabanda ambayo yalishehenezwa na
kazi mbalimbali za watoto zikiwemo; - picha za kuchora, vifaa vya kufinyanga
kwa udongo (kinu na kibao cha kusukumia chapati), bangili za wanawake za
kuvaa mikononi ambazo hutengenezwa na watoto wenye ulemavu wa macho.
5 Hitimisho
Kila mmoja wetu awajibike kwa nafasi aliyonayo katika kuhakikisha tatizo la
watoto wanaoishi mitaani linatoweka na hatimaye kuwa na Taifa endelevu lenye
kutekeleza na kusimamia misingi ya haki na wajibu kwa watoto.

chadema cha alika wagombe wa uchaguzi 2015
Katika jitihada za kujiandaa na uchaguzi mkuu wa 2015 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka wanachama wake wenye nia ya kugombea ubunge na udiwani kuwasilisha barua za maombi, picha, vyeti, wasifu na jimbo wanalotaka kugombea kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu, tayari kwa maandalizi.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema jana na kuwaagiza wanafunzi ambao ni wanachama wa Chadema wanaohitimu mwaka huu katika vyuo vikuu vya Mkoa wa Dodoma kufanya hivyo mara moja.
Akihutubia katika mahafali ya kuwaaga wanachama hao wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma, St. John’s na Chuo cha Biashara (CBE), Mbowe, alisema kila anayetaka kugombea awasilishe maombi na kwamba mwaka 2015 wagombea watakuwa wengi kwa kila jimbo ili kuleta ushindani.
Alisema taarifa za wagombea hao zitafanywa kuwa siri na watakaojitokeza kugombea 2015 watapata mafunzo maalumu ya uongozi, kampeni na pia watapewa ajenda za kuzungumzia majukwaani wakati wa kampeni.
“Kama CCM ilidhani kuwa mwaka 2015 kutakuwa na jimbo au kata ambalo mgombea atapita bila mgombea, safari hii wameula wa chuya. Tumefanya operesheni Mtwara na Lindi, tutaendelea na operesheni Dar na Pwani kisha tutaendelea Dodoma, Morogoro na Singida.
“Tunataka kujenga mtandao wa chama ngazi za chini, vijijini na mtaani kama CCM inadhani tunacheza makidamakida watashangaa,” alisisitiza Mbowe na kuongeza kuwa lengo ni kuwatambua na kuwajenga viongozi mapema.
Katika mkutano huo, Mbowe aliwaambia wanachama wa Chadema vyuoni (Chaso) Mkoa wa Dodoma kuwa CCM inawanyanyasa wanafunzi wanaoiunga mkono Chadema na pia inanyanyasa wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoonekana kushabikia chama hicho.
MIKAKATI YA CHADEMA
Mbowe ametangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 Chadema haitapokea 'maskrepa' yaliyokosa nafasi katika vyama vingine, biashara ya kupokea watu waliokosa nafasi katika vyama vingine ilikuwa 2010.
Alisema tabia ya kukimbilia meli dakika za mwisho ilikuwa zamani na kwamba uchaguzi ujao hawatakubali waliokosa fursa kwa vyama vyao kukimbilia Chadema.
Mipango yao ni kupata wabunge na viongozi bora watakaopimwa kwa dhamira, uwezo na uwajibikaji kwa chama.
“Wafanyakazi wanatishiwa kufukuzwa kazi na wafanyabiashara wanafilisiwa na kubambikiwa kodi kisa wameonekana kushabikia Chadema,” alisema.
Baada ya kuhutubia, wanachama wa Chadema vyuoni mkoani Dodoma wameutaka uongozi wa chuo kuondoa bango la CCM lililoko UDOM kwa maelezo kuwa ni kinyume cha Ibara ya 7 ya Sheria ya Vyuo Vikuu ya 2005.
Akisoma risala ya wanafunzi Pasquina Ferdinand mwanafunzi wa Shahada ya Ualimu mwaka wa pili, Chuo Kikuu cha St John’s, alisema CCM ina bango ndani ya UDOM kinyume cha sheria ya vyuo vikuu ya 2005, alionyesha kuwa ni sheria inayoihusu Chadema pekee lakini kwa CCM haina tatizo.
“Tunaomba umweleze Waziri Mkuu kama siasa haziruhusiwi vyuoni kwanini basi CCM ina bango UDOM kinyume cha sheria wapewe amri ya kuliondoa kwani UDOM siyo mali ya CCM inajengwa kwa fedha za Watanzania,” alisema.
Akijibu, Mbowe aliwataka wanafunzi wanachama wa Chadema wanaosoma UDOM kumletea taarifa za kunyanyaswa kwa itikadi yao ili azipeleke kwa Waziri Mkuu na awe na ushahidi wa kutosha ili amuulize swali bungeni.
Wakati huo huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Tundu Lissu, ametangaza kuwa watatumia nguvu ya umma kupinga kufukuzwa wanafunzi vyuo vikuu.
“Sisi wazazi tunawajibika kuhakikisha kuwa watoto wetu wanasoma kwa kuizuia serikali isiwanyanyase kwa kuwafukuza wakidai haki yao, hili litafanywa kwa njia ya nguvu ya umma ... tukiona wanafunzi wamefukuzwa UDOM umma uingie mitaani kuandamana kama ni Dar es Salaam watu waingie mitaani tuhakikishe kuwa hapatoshi,” alisema Lissu.

CHANZO: NIPASHE
na Henry Kapinga blog
Friday, June 15, 2012
katiba
Watanzania washauriwa kutumia fursa waliyonayo sasa ya kuchangia maoni ya katiba mpya ya Jamhuri ya Tanzania ambayo hawajawahi kupata tangu miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania, kwa sasa serikali imeamua kusikia na kujibu kilio cha Watanzania kutaka kuunda katiba mpya inayoshirikisha mawazo ya wananchi badala ya kutumia katiba ambayo iliundwa na wananchi wachache.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Mlimani Media, Bi. Edda Sanga wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi
Subscribe to:
Posts (Atom)