Waumini
wa kanisa la Pentekoste Holiness Association Mission in Tanzania pamoja na
wachungaji wa makanisa jirani na kijiji cha Iyunga Mapinduzi, wilaya ya Mbeya
vijiji, jijini Mbeya wamefanyia ibada ibada katika eneo la choo baada ya
mshirika wa kanisa hilo kuingia katika choo hicho na kukuta kimejaa nguo,
madumu na chupa zenye damu pamoja na nyama zinazosadikiwa kuwa za binadamu na
wanyama.
Kwa
mjibu wa shuhuda watukio hilo la namna yake Eliza Subiri amesema aliingia katika choo hicho kwa lengo
la kujisaidia ndipo akaiona chupa katika shimo la choo, jambo lililomsababisha
aende kwa mchungaji wa kanisa hilo na kumwambia kile achokiona.
Kama
maigizo vile, baada ya mchungaji kuingia katika choo hicho akashuhudia mengi
zaidi ya vile alivyoviona muumini huyo. Mchungaji na shuhuda wa tukio hilo
waliamu akuripoti tukio hilo kwa majirani na serikali ya kijiji hicho.
Tukio
hilo la namna yake limewaunganisha wachungaji na waumini wa makanisa zaidi ya
matano na kufanya Ibada ya pamoja kwa ajili ya maombezi katika eneo hilo.
Kwa
upande wao wachungaji waliofanya mahojiano na blogu hii wanazungumziaje
tukio hilo?
Bofya hapa uwasikilize....
https://soundcloud.com/user442431332/wachungaji?in=user442431332/sets/habari-kuhusiana-tukio-la-choo
wachungaji na waumini kwa pamoja leo
walikubaliana kuchoma moto vitu hivyo, lakini serikali ya kijiji hicho
imewazuia wasichome moto leo na hivyo kuwataka kesho wachome mto vitu hivyo kwa
kushirikiana na serikali ya kijiji hicho.
Nao
mashuhuda walioshuhudia maajabu hayo wametoa ushuhuda wao na kuwaasa watanzania
kumtegemea Mungu kwa moyo wote na kwa kila jambo kwa kuwa siku za mwisho
zimekaribia.
Moja
ya mashuhuda hao Lone Mkono amesema matukio kama hayo yanaashiria mwisho wa
dunia na kuwataka wakristo wasife moyo kwa sababu ya majaribu wanayo yapata.
Kwa
mjibu wa mchungaji mwenyeji wa kanisa hilo amesema mara nyingi kanisa hilo tangu
lijengwe limekuwa likiangukaanguka kuta zake mara kwa mara, hivyo na tukio hilo
ameliunganisha na matukio mengine yanayolikabili kanisa hilo kuwa ni mipango ya
shetani kutaka kulirudisha nyuma kanisa hilo.
Bofya hapa kupata sauti za mashuhuda wachungaji na mchungaji mwenyeji kasema nini
No comments:
Post a Comment