Serikali imetangaza matokeo ya darasa
la saba ambapo watahiniwa wamefaulu 427, 606 kati ya watahiniwa 867,983 na watahiniwa 13
wamefutiwa matokeo ya mtihani kutokana na udanganyifu katika mtihani huo.
Akiongea na waandishi wa habari kaimu
katibu mtendaji wa baraza la mitahani, Dk. Charles Msonde amesema wastani wa
kufaulu umeongezeka kwa asilimia 19.89 ukilinganisha na mwaka jana(2012) ambapo wastani wa kufaulu ulikuwa asilimia
30.72.
Msonde amesema jumla ya watainiwa
walikuwa 867,983, waliopata daraja la A-C ni watahiniwa 427,606 ambapo ni
wasichana 208,227 na wavulana 219,379, wakati watahiniwa waliopata daraja D ni
389,948, wavulana 166,010 na wasichana ni 223,9938 na daraja E ni watahiniwa
27,367 ambapo wavulani ni 13,425 na wasichana ni 13,942.
Ameongeza kuwa watahiniwa mwaka huu
wamefaulu zaidi somo la Kiswahili kwa asilimia 60 na somo ambalo wamefaulu kwa
kiwango cha chini ni somo la Hisabati ambapo wamefaulu kwa asilimia 28.62
ikilinganishwa na matokeao ya mwaka 2012.
Sambamba na hili, baraza la Mitihani
Tanzania limefuta matokeo yote ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE),
2013 ya watahiniwa 13 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.
Aidha, amesema Baraza la Mitihani la
Tanzania limewasilisha matokeo hayo kwenye Mamlaka husika ili zifanye uchaguzi
wa watahiniwa wa kujiunga na elimu ya Sekondari.
Kwa upandu mwingine Msonde amesma
Baraza la Mitihani la Tanzania kwa kujiridhisha na usahihi shaji kwa kutumia
mfumo wa kompyuta (Optical mark Reader (OMR), Balaza lilitenga sampuli ya
karatasi 20,795 ya majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka katika wilaya 48 za
mikoa 9; Iringa , kagera, Shinyanga, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga
ambazo zilisahihishwa kwa mkono na baadaye kufanya ulinganifu na usahihishaji
wa OMR na kubaini kuwa mfumo wa kutumia kalamu kusahihisha ulikuwa na makosa ya
kibinadamu kwa asilimia 1.2.
PICHA KUTOKA kIONGOZI BLOG
Mfumo wa kusahihisha Mitihani kwa
kutumia mfumo wa kompyuta OMR ulianzishwa na Baraza la mitihani la Tanzania
toka mwaka 2012 ambao umesaidia kupunguza idaidi ya washiriki wa usahihishaji
kutoka washiriki zaidi ya 4000 hadi 302.
No comments:
Post a Comment