A
|
skofu
msaidizi wa Jimbo la Kinondoni na Mchungaji
wa kanisa la EAGT Mikocheni ‘A’ Filipo Phiri apiga marufuku kwa waumini
wote uvaaji wa nguo fupi, mlegezo na unyanyuaji matiti kwa wanawake na mavazi yasiyoendana
na misingi ya dini pamoja na utamaduni
wa Mwafrika, asema yarudisha nyumba Injili ya Kristo.
Akihutubia
waumini wa kanisa hilo lililopo Samaria Mikocheni A Desemba 22 mwaka huu,
mchungaji Phiri alisema wakristo wanaovaa nguo fupi hawana nia ya kukuza injili
kwa mataifa zaidi ya kuwaingiza majaribuni waumini wenzao na hata mataifa
wanaotaka kuwahubiria na hivyo kuwa kikwazo katika kueneza injili ya Yesu
Kristo kwa Mataifa.
Aliongeza
kuwa wanawake wanatakiwa kuvaa nguo fupi (nusu uchi) wakati wakiwa na wanaume
zao katika maandalizi ya tendo la ndoa
na si kuvaa nguo fupi kanisani kila mahali kwa kuwa huhizi heshima zao.
Pia,
mchungaji Phiri alikemea tabia ya wanawake kunyanyua matiti yaonekane juu kwa
madai kuwa (wasichana) wengi hawataki yaonekane matiti yao yameanguka
(yamelala) jambo ambalo mchungaji alidai limekuwa likiwaingiza vijana majaribuni
kwa kuwatamani wasichana hao pindi wakiyaangalia matiti (maziwa) ya wanawake hao.
“Tabia
ya kuacha maziwa yenu yaonekane kwa watu, na kunyanyua maziwa yenu kwa kuvaa kanchiri
(sidiria) ndogo si desturi yetu walokole wala Waafrika bali mmeiga tu.
“Nikimwona
mwanamke amevaa nusu uchu au nguo vupi, amenyanyua maziwa kuwatega vijana wangu
nitamfukuza mbele ya kanisa hata kama yupo kutoa sadaka madhabahuni,”
alisisitiza mchungaji Phiri.
Aidha
Mchungaji Phiri aliwataka vijana wanaovaa suruali mlegezo maarufu kata ‘K’
kuacha tabia hiyo mara moja vinginevyo nao atawafukuza kanisa akidai kuwa nao
wanazui in jili ya Yesu Kristo isisonge mbele kwa kuwa mlegezo huvaliwa na watu
wasiokoka na waliokosa heshima mbele za watu.
“Nikikuona
umevaa mlegezo makalio yako yanaoneka ama chupi yako inaonekana, I cannot
tolerate you, I chase you out (siwezi kukuvumilia, nitakifukuza),” mchungaji
Phiri aliwasisitizia vijana waliookoka.
Hata
hivyo, mchungaji Phiri aliwataka wanaume kukaa na wake zao na kuwaonya juu ya
mavazi wanayovaa mbele za watu na kuwaambia kuwa wajue kuwa mwanamke anatakiwa
kuonesha mapaja, maziwa yake kwa mwanamume wake tu, na kwa watu wengine
mwanamke anatakiwa kusetiri mwili wake kwa mavazi.
Vivyo
hivyo, kwa wanaume aliwatakiwa kutoacha vifua wazi, kuvaa kaptura akidai kuwa
si tabia ya watu waliookoka kuvaa mavazi yayowavunjia heshima mbele za watu.
Hayo
yote aliongea wakati akifundisha somo la MSIMAMO WA WOKOVU akisoma Mathayo 7:
24-27, Yuda 1:3-5 na 1Wakorintho 2:4-8
Bofya link hii ukitaka sauti
https://soundcloud.com/user442431332/filipo-phiri-nguo-fupi-matiti
Bofya link hii ukitaka sauti
No comments:
Post a Comment