NGUVU YA HABARI

Thursday, December 27, 2012

Uchumba ni Mkataba na Ndoa ni Agano.

Ndoa ni agano ambalo mtu akisha kuaga ama kusaini makubaliano ya kuoana hayo, haruhusi kumwacha mke ama mume, lakini uchumba  ni makubaliano ya awali ambayo msichana na mvulana hukubaliana kwa malengo ya kuja kuoana baadaye.
makubaliano haya huwa ni mkataba wa watu wawili na makubaliano hayo husainiwa kama wa mkataba ikiwana na maana kwamba mmoja akimchunguza mwenzake wakati wa uchumba akagundua kuwa ana kasoro na hawezi kumfaa katika ndoa, huamua kuvunja mkataba huo na kutafuta mwingine.
lakini mume ama mke akimwacha mwenzake na kuolewa na mwingine ama kuoa mwingine huitwa mzinzi na huhesabika ametenda dbambi.

lakini zifuatazo ni sababu zinazo changia kuvunjika kwa uchumba:                                           

1. Kukosekana kwa uaminifu na uvumilivu kwa wachumba wenyewe katika mahusiano yao. Pindi wachumba hawa wanaposhindwana kuaminiana na kuvumilia, kati yao mmoja huamua kutafuta akiba ama service account na kumwona mwenzake kama hafai tena bila kumshirikisha katika masuala anayoona hayeendi sahihi katika mahusiano yao. Uongo hutawala na sababu nyingi zisizo za msingi ambazo hufungulia mlango wa shetani kuwashambulia na hatimaye uchumba kuvunjika.

2. Uchumba wa mali ama uchumba wa mwenye nacho tu: Kama wachumba hao wanakuwa wamependana kwa sababu mmoja wao anauwezo fulani wa mali ambao umeshawishi mmoja wapo akubaliane na kuwa na mahusiano ya uchumba, pindi mmoja huyo anapofilisiki basi hatima ya uchumba huo huvunjika na mwenye roho ya kutamani watu wenye  nacho basi huanza kupepesa macho na kumtafuta mtu mwingine mwenye nacho. 

Hali ya kutamani maisha makubwa ambayo ni nje na uwezo husababisha uchumba kuvunjika na wakati mwingine akijitokeza mtu mwingine ambaye anaonyesha dalili fulani za kuwa na mali au pesa zaidi ya yule mchumba huchangia kuvunjika kwa uchumba  hivyo ni vizuri kulidhika na mchumba wako na mwenzi uliyenaye kwani MUNGU atawabarikia mkiwa pamoja.                                             

 3.Kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa (katika kipindi cha uchumba). Mara nyingi wachumba wengi wanapendas kufanya ngono katika kipindi cha uchumba hali ambayo huhatarisha mahusiano ya wachumba. kwa maana mtu anayefanya ngono kabla ya kuolewa ni sawa na mtu anayeonjesha parachichi mojawapo kati ya maparachichi anayouza ili mteja aonje utamu wa maparachichi hayo, na akisha kuonja parachichi hilo huwa hanunui lile alilo onja badala yake hununua ambalo hakijaonjwa. Vivyo hivyo mwanamke anayefanya ngono kabla ya ndoa ni rahisi kuachwa ukilinganisha na yule anayetunza kiapo.

Kumbuka uasherati ni dhambi na pia kufanya ngono kabla ya ndoa kunasababisha watu kuzoeana na kumtambua udhaifu mwenzake na hivyo kuamua kuvunja uchumba na kumtafuta mwingine kwa kigezo kuwa atampata mwenye afadhali kuliko wa kwanza.

NI DHAMBI KWA WACHUMBA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA

4.Kujitangaza mapema kwa watu kabla ya wakati muafaka. kujitangaza kwa wachumba kwa jamaa zao kabla ya muafaka, hutoa fursa kwa baadhi ya watu kuzua maneno ya uchonganisha na ya kukatisha tamaa kati ya hao wachumba.

Mfano, wafi watarajiwa wanaweza kumwambia kaka yao amechagua mwanamke asiye na mvuto ama ana sura ya kufukuza watu halia ambayoa kama mwanaume hana msimamao wa kuwakemea dada zake ama marafiki zake, basi huamua kuachia ngazi, vivyo hivyo kwa mwanamke na huchezeshwa sebeni na wasichana wenzake wenye husuda naye ama kila mtaa wanajua yaani kila mtu anajua hii husababisha mmoja ya wachumba kuona kuwa huyu mwenzangu hana siri na hawezi kutunza mambo huenda hata tutakapooana hataweza kutunza siri.

hivyo huchukua hatua ya kuvunja uchumba na wakati mwingine kusemasema kabla ya muda huwasababisha wale walio maadui zenu kuwazunguka kwa mbele na kupindua mathalani marafiki wa karibu wana weza kuzunguka na kukugeuzia kibao hatimaye mjoja wapo hikuta rafiki anamshawishi avunje uchumba na  ya siku chache huyo huyo mshauri anamvisha pete mchumba wako. 

5.Kufuata ushauri bila kuupima na kutomsikiliza MUNGU. Hii inaweza kusababisha  uchumba kuvunjika. ni vizuri kujifunza kumsikiliza MUNGU juu ya yule aliye kuongoza kwamba atafaa kuwa mwenzi wako wa ndoa badala ya kuwasikiliza watu wanasema nini juu ya wewe na mchumba wako. watu wanaweza kumtoa kasoro mfano mchumba mwenyewe hajasoma,ni mbaya,hana figa nzuri,mchafu,hamuendani, maskini na kasoro nyingi tu na hiyo husababisha uchumba kuvunjika                                                     

6.Kuparamia uchumba bila kumhusisha MUNGU. Watu wameonana siku moja na kutamaniana bila kuchunguzana ama kumhusisha MUNGU wanachumbiana. Baada ya muda mfupi wanatangaza mipango ya kuoana kwa kwa watu. Na pindi mmoja wapo anapogundua kuwa walikurupuka basi wala MUNGU hakuhusika kabisa  katika mchakato mzima wa uchumba wao, basi matokeo yake uchumba huvunjika. 

7.kutumia muda mwingi katika uchumba kabla ya ndoa. Kuna baadhi ya wachumba wanatumia muda mwingi sana kukaa katika mahusiano ya uchumba kwa malengo ya kusomana tabia au kuchunguzana au kusubiriana katika masomo nk. Hali hii hupelekea kuchokana katika mahusiano na kuwasababishia kuona kama huenda labda nilichagua mtu asiye sahihi. Baada ya kusoma na madhaifu mengi kwa muda mrefu mwisho uchumba huweza kuvunjika.                                                                                                      

8. Kutofautiana kwa imani ama Dini: Aidha wachumba wanaochumbia wenye msimamo tofautiwa dini husababisha uchumba wao kuvunjika pindi mmoja wapo anapogoma kuhamia kwenye dini ya mwenzake.

9.Upinzani wa shetani ili ukose kilicho bora zaidi. Kuvunjika kwa uchumba wakati mwingine kunaweza kusababishwa na ibilisi shetani ambaye ni mdau wa kwanza wa upinzani juu ya mafanikio ya wana wa MUNGU. Ndiyo maana tunahitaji  sana kufunga na kuomba ili kuvunja na kuharibu kazi za shetani na mipango aanayotuwazia sisi katika maisha yetu.

SHETANI ALIWADANGANYA ADAMU NA EVA  KWA SABABU HAPENDI MAFANIKIO KWA WANA WA MUNGU    

10.Uchumba kuvunjika kwa sababu ya mapenzi ya MUNGU.Sio kila kitu kinaweza kusababishwa na shetani, wakati mwingine MUNGU mwenyewe huingilia kati na kusababisha uchumba fulani kuvunjika kutokana na sababu za kimungu ambazo wakati mwingine kwetu sisi sio rahisi kuweza kuzijua kwa haraka mpaka wakati kamili wa MUNGU utimie au kusudi lake kujidhihirisha wazi. Ni vizuri kwetu sisi kama watu wa MUNGU kutafuta mapenzi ya MUNGU na kujua kwamba kuna wakati  MUNGU mwanyewe  anaweza kusababisha uchumba  kuvunjika kwa ajili ya usalama wetu.

MUNGU BABA AKUBARIKI SANA

No comments: