NGUVU YA HABARI

Thursday, September 27, 2012

TANZANIA SI NCHI MASIKINI

puuzieni usemi kuwa tanzania ni nchi masikini


Green tea carpet
watanzania wameshauriwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu wa kazi mbalimbali zinazoweza kuwasaidia kuondokana na hali ngumu ya maisha na kuachana na tabia ya majungu na manunguniko na badala yake wajitume kufanya kazi.

hayo yamesemwa na mchungaji wa kanisa la Evangelical Assembles of God, Pontian Kaganda lililopo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam-Mlimani wakati akihubiri kanisani hapo.

Kaganda amesema baadhi ya watanzania hususani vijana hawapendi kubuni kazi za kufanya badala yake wamekuwa kipaumbele kukaa vijiweni na kuilaumu serikali yao wakidai haiwapatii ajirana kuzidi kunung'unika huku wakiridhika na usemi wa wapotoshaji wa Tanzania ni nchi masikini.

hata hivyo Kaganda amewataka Watanzania kuupuuzia usemi huo kuwa Tanzania ni nchi masikini, huku akisema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na maliasili nyingi ambazo kama watanzania watazitumia vizuri  wataweza kujikomboa na hali ngumu ya maisha.

Ameongeza kuwa watu wengi wanaonja machungu ya maisha yao kutoka tu na baadhi ya watu kujilimbikizia mali za nchi kwa manufaa yao binafsi na kuzidi kuhujumu uchumi wa nchi kwa kuzidi kufisaidi mali ya ummma.

Aidha amewataka watanzania hususani vijana kutumia elimu waliyonayo kubuni biashara yo yote ama kulima kilimo bora ambacho kitawawezesha kujipatia kipato na kuondokana na hali ngumu ya maisha na kutatua tatizo la ajira. 

Kaganda amesisitiza kuwa hali ngumu ya maisha itondoka iwapo watu wenyewe watajituma kufanya kazi kwa bidii na kuunda vikundi ili waweze kupata mikopo serikalini na kwenye banki kuliko kwenda kukopa mtu mmoja mmoja.

Kilimanjaro with snow from Swissair