NGUVU YA HABARI

Friday, November 22, 2013

"WATANZANIA FUNGUENI MIRADI YA BIASHARA, ACHENI KULALAMIKA": Mchungaji Filipo Phiri

Watanzania wametakiwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kibiashara na kuachana tabia ya kutegemea mishahara na kuepuka kumkosea Mungu kwa kunung’unika kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu na kumtolea Mungu.

Askofu msaidizi wa jimbo la Kinondoni na mchungaji wa kanisa la EAGT lililopo Mikocheni A jijini Dar es Salaam, Filipo Phiri amewataka Watanzania kufanya biashara yo yote halali itakayo waingizia kipato badala ya kuwa tegemezi wa mishahara kwa walioajiriwa.
Mchungaji Phiri amesema wakiristo wanapokuwa na miradi yao ya biashara mbalimbali ni rahisi kwao kumtumikia mungu kwa moyo kwa kuwa atakuwa na fedha ya kumtolea Mungu, michango ya kanisa na pamoja na fesha za kuendeshea maisha yake.
Mchungaji Phiri amesema kutokana na kukosa fedha waumini ajikuta wakishindwa kumwabudu Mungu ipasavyo pale wanapo ona wenzao wakitoa sadaka na kulipa michango ya kanisa.
Picha imechukuliwa kwenye http://www.google.co.tz/imgres?imgurl=http://cdn.charismanews.com/images
Sambamba na hilo mchungaji Phiri, amewataka wakristo kuwa na upako mpya kila siku unaoleta mzigo na ari ya kimtumikia Mungu bila kuteteleka waingiapo majaribuni.
Mchungaji Phiri ametumia kitabu cha 1Samwel 17:20-45, kuonesha namna Mungu alivyompa nguvu za mtumishi daudi za kumuua Goliathi kwa sababu alipakwa mafuta na ajiweka tayari kila saa kwa kumtumikia mungu.

No comments: