Wakristo nchini Tanzania wametakiwa
kusherehekea Sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu
Kristo kwa kuwasaidia wasiojiweza kuashiria kuwa wanatambua maana ya Krismasi
na umuhimu wake kama Mungu alivyomtoa mwanae Yesu Kristo kwa ajili ya
kuwakomboa wanadamu mikononi mwa shetani.
Mchungaji wa Kanisa la Elimu Pentekoste
lililopo Airport jijini Mbeya, Jerome
Steven Saninga akihojiwa na mwandishi wa blogu hii na radio Mlimani alisema
wakristo wanatakiwa kuzingatia umuhimu wa kuzaliwa kwa Yesu kristo na kutenda
matendo yaipasayo injili ambayo Mungu aliwatendea wanadamu kwa kumtoa Mwana
wake wa peke Yesu Kristo azaliwe duniani kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu.
Mchungaji Saninga alisema wakristo
wanatakiwa kuadhimisha Krismasi kwa kupinga na kulani vitendo vyote vilivyo
kinyume na mpango wa Mungu kama vile mauaji, ubakaji, ulevi kwa kuhubiri Injili
ya Yesu Kristo kwa imani na matendo.
Naye Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia ni Mbuge wa Jimbo la Iringa Mjini
(CHADEMA) alipohojiwa kwa njia ya
Simu alisema ni wakati mzuri kwa Watanzania na wakristo kwa ujumla wakatumia
kipindi hiki cha Krismas kuwasaidia watoto yatima, wajane na wagonjwa waliopo
hospitalini na majumbani baadala ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa mambo ya
anasa kama vile kulewa.
“Tunasherehekea Krismasi hii lakini
kila mtu kwa mmoja mmoja atafakari Kwamba hakuja duniani kwa bahati mbaya na
aone ni aibu kwa kufa na anazikwa bila mchango wa maana kwa jamii.
“Ni wakati mwafaka wa kuonesha upendo wako
kwa watu badala ya kufanya mambo ambayo ni kinyume kabisa na maneno ya Mungu na
pia kuonesha upendo kwa jamii inayotuzunguka kama vile kutembelea yatima na
wagonjwa wapo hospitalini,”
Kupata sauti ya Mchungaji Msigwa bofya hapa............https://soundcloud.com/user442431332/mchungaji-msigwa-ahimiza
Nini
Maana ya Krismasi?
“Krismasi ni kati ya Sikukuu mojawapo
ambazo huadhimishwa na Wakristo ulimwenguni kote wakikumbuka siku ya kuzaliwa
kwake Yesu Kristo ambaye alizaliwa ili
kumkomboa mwanadamu mikononi mwa adui shetani
aliyekuwa akiwatawala wanadamu na kuwatenga wanadamu hao na Mungu wao kwa sababu ya dhambi wazitendazo,”
Mchungaji saninga alitoa maana ya krismas.
Mchungaji Saninga akiombea maji wakati wa kubatiza waongofu wapya mkoani Mbeya |
Aidha, Mchungaji Saninga aliwaasa wakristo kuonesha upendo wa dhati katika
kipindi hiki cha Krismasi kwa kuwa wanaadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mwokozi
wa wanadamu na kuachana na mambo ya anasa kipindi hiki cha Sikukuu.
Kupata Sauti ya Mchungaji Saninga Bofya hapa............................https://soundcloud.com/user442431332/mchungaji-saninga-mahojiano
Naye Mchungaji Peter Msigwa alisema Krismasi ni siku ambayo baadhi ya
Wakristo huadhimisha Kila ifikapo tarehe 25 mwezi Disemba kama ishara ya
kukumbuka miaka 2000 iliyopita ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambayo ni Mkombozi
wa ulimwengu baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika Bustani ya Edeni na
kutengana na Mungu.
“Krismas ni mwanzo wa ukombozi wa
mwanadamu ambao hukamilishwa na ufufuo wa Yesu Kristo”.
Je,
ni kweli Yesu Kristo alizaliwa tarehe 25 mwezi wa 12?
Akijibu swali hilo Mchungaji Saninga
alisema si kweli kuwa Yesu alizaliwa tarehe 25 mwezi wa 12 bali ni tarehe
ambayo wanathiologia walikaa na kukubaliana iwe siku ya kuadhimisha kuzaliwa
kwa Mwokozi wao Yesu Kristo kama ishara ya kutambua umuhimu wa kuzaliwa kwake.
Aliongezakuwa waafrika wanasherekea
Sikukuu hii kwa kufuata Kalenda za Wayahudi ambayo alidai wana kalenda mbili,
kalenda ya Kidini na kalenda ya kiserikali tofauti na waafrika ambao wanatumia
kalenda moja waliyoridhishwa na wakoloni.
“Ni vema mkristo au mtu ye yote
akaruhusu Yesu kristo azaliwe ndani ya moyo wake, na hili ni jambo linalotakiwa
kufanyika kama ilivyoandikwa katika Ufunuo 3:20; Tazama, nasimama mlangoni
nabisha. Kama mtu ye yote akisikia sauti Yangu na kufungua mlango, nitaingia
ndani na kula pamoja naye,naye pamoja name,” alisema mchungaji Saninga.
Hata
hivyo mchungaji Saninga amewataka Wakristo kusherekea sikukuu ya Kuzaliwa kwa
Yesu Kristo (Krismas) kwa kuangalia umuhimu wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambaye
alikuwa kufanya suluhu la ukombozi wa mwanadamu baada ya mwanadamu kujitenga na
Mungu kwa sababu ya dhambi.
Krismasi ni sikukuu ambapo Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa
tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe6 Januari katika ule wa mashariki
Hata hivyo kwa mjibu wa http://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi#Historia_ya_Krismasi inaonesha kuwa hakuna tarehe halisi ya
kuzaliwa kwake Yesu Kristo kutokana na
kutojulikana utamaduni wa Wayahudi kuhusiana na kukumbuka siku ya kuzaliwa
kwake.
Hata hivyo vitabu vya historia ya
Kristo vinaonesha kuwa Sikukuu ya Krismasi ilianzishwa na nchi ya Roma na
mataifa ya kati ambayo yalikuwa na hamu ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi
wao na baadaye mataifa mengine yakaunga mkono.
Habari nyingine zinadai kuwa Krismasi
ilikadriwa na wataalamu wa nchi ya Misri ambao walidai kuwa kikundi cha
wakristo wa Basilides wa Misri waliosherehekea siku ya kuzaliwa Kristo tarehe 6
Januari kila mwaka na wengine wakikadria tarehe 25 mwezi Desemba.
No comments:
Post a Comment