'Mali bila daftari hupotea bila habari' Ndivyo ninavyoweza kusema kuhusiana na somo la TEHAMA-TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO linavyo fundishwa nchini Tanzania hususan maeneo ambako hakuna nishati ya umeme.
Wanafunzi wanamezeshwa nadharia kuhusiana na matumizi ya komputa, huku wakiwa hawajui kompyuta yenyewe ipoje, na watawezaje kutambua vifaa vyake kwa kuangalia picha ambazo zinaonesha sehemu mojawapo tu ya uso?
cha kushangaza zaidi baadhi ya walimu wenyewe wanaofundisha shuleni huko hawazijui kompyuta zilivyo zaidi ya kukariri vitabu na kuingia kumkaririsha mwanafunzi.
Je, tunataka tuandae wanasayansi wa namna gani nchini Tanzania? Wanasayansi wa vitabuni tu wasio jua kutumia elimu waliyopata kwa vitendo?
Je, nani wa kulaumiwa katika mfumo huu mbovu wa kufundisha TEHAMA kwa nadharia wakati ni somo la vitendo?
Je, serikali ili kurupuka kuingiza somo hili katika mtaala bila kufanya utafiti? serikali haina budi kuangalia upya ili kupata