NGUVU YA HABARI

Saturday, September 17, 2016

KILIMO: WAKULIMA WA KAHAWA BADILISHENI AINA ZA MBEGU

Na Laudence Simkonda, Mbeya

Wakulima wa zao la Kahawa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wametakiwa kubadilisha mfumo wa uzalishaji wa zao hilo, kwa kuachana na kilimo cha zamani cha kutumia mbegu za asili na badala yake waanze kupandanda Mbegu za Kisasa.

Kwa mujibu wa Afisa ugani Lized Cope, Miongoni mwa mbegu zilizopendekezwa kutumiwa ni kahawa aina Compact inayozalishwa na taasisi ya utafiti wa mbegu Tanzania ambayo inadaiwa kuwa inaongeza thamani ya zao hilo.


Mojawapo ya mbegu za kahawa zinazodaiwa kustawi vizuri Wilayani Rungwe
Aidha amesema wakulima wengi wa Kahawa ndani ya wilaya hiyo, bado wanaendesha kilimo cha kizamani, kwa kutumia begu walizo rithi kutoka kwa mababu zao.

Kwa upande wao wakulima wa wilaya hiyo wamesema utitili wa kodi ya ushuru, ukosefu wa soko la uhakika na miundombinu mibovu ya barabara ni changamoto nyingine ambayo inawakatisha tamaa wakulima.

Hata hivyo, Meneja shirika la HNRS Richard Mbaga na Mwenyekiti Halmashauri ya Rungwe Ezekiel Mwakota wameyataka Mashirika binafasi kwa kushirikiana na Serikali ya wilaya kuhamasisha wakulima kuongeza juhudi za uzalishaji wa zao hilo.