Wakulima
wa zao la Kahawa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wametakiwa kubadilisha mfumo wa
uzalishaji wa zao hilo, kwa kuachana na kilimo cha zamani cha kutumia mbegu za
asili na badala yake waanze kupandanda Mbegu za Kisasa.
Kwa
mujibu wa Afisa ugani Lized Cope, Miongoni mwa mbegu zilizopendekezwa kutumiwa
ni kahawa aina Compact inayozalishwa na taasisi ya utafiti wa mbegu Tanzania ambayo
inadaiwa kuwa inaongeza thamani ya zao hilo.
Mojawapo ya mbegu za kahawa zinazodaiwa kustawi vizuri Wilayani Rungwe |
Kwa
upande wao wakulima wa wilaya hiyo wamesema utitili wa kodi ya ushuru, ukosefu
wa soko la uhakika na miundombinu mibovu ya barabara ni changamoto nyingine
ambayo inawakatisha tamaa wakulima.
Hata
hivyo, Meneja shirika la HNRS Richard Mbaga na Mwenyekiti Halmashauri ya Rungwe
Ezekiel Mwakota wameyataka Mashirika binafasi kwa kushirikiana na Serikali ya
wilaya kuhamasisha wakulima kuongeza juhudi za uzalishaji wa zao hilo.
No comments:
Post a Comment