Dereva wa pikipiki Braison Mlonganile mkazi wa kijiji cha Nyumbo kata ya Ikuna mkoani Njombe ameuwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa mtoni.
Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi mkoani humo lina washikilia watu watatu akiwemo mwanamke mmoja wakihusishwa na tukio hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa mwili wa marehemu Braison Mlonganile umekutwa mtoni ukiwa na majeraha sehemu ya shingo yake.
Kamanda Mtafungwa alisema jeshi la polisi linatoa wito kwa raia kutojihusisha na matukio ya mauaji na kusema kuwa watii sheria bila Shuruti na kuwa watu wa kwanza kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment