Watanzania wametakiwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kibiashara na kuachana tabia ya kutegemea mishahara na kuepuka kumkosea Mungu kwa kunung’unika kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu na kumtolea Mungu.
Askofu msaidizi wa jimbo la Kinondoni
na mchungaji wa kanisa la EAGT lililopo Mikocheni A jijini Dar es Salaam,
Filipo Phiri amewataka Watanzania kufanya biashara yo yote halali itakayo
waingizia kipato badala ya kuwa tegemezi wa mishahara kwa walioajiriwa.
Mchungaji Phiri amesema wakiristo
wanapokuwa na miradi yao ya biashara mbalimbali ni rahisi kwao kumtumikia mungu
kwa moyo kwa kuwa atakuwa na fedha ya kumtolea Mungu, michango ya kanisa na
pamoja na fesha za kuendeshea maisha yake.
Mchungaji Phiri amesema kutokana na
kukosa fedha waumini ajikuta wakishindwa kumwabudu Mungu ipasavyo pale wanapo
ona wenzao wakitoa sadaka na kulipa michango ya kanisa.
Sambamba na hilo mchungaji Phiri,
amewataka wakristo kuwa na upako mpya kila siku unaoleta mzigo na ari ya
kimtumikia Mungu bila kuteteleka waingiapo majaribuni.
Mchungaji Phiri ametumia kitabu cha 1Samwel 17:20-45, kuonesha namna Mungu alivyompa nguvu za mtumishi daudi za kumuua
Goliathi kwa sababu alipakwa mafuta na ajiweka tayari kila saa kwa kumtumikia
mungu.