NGUVU YA HABARI

Saturday, November 2, 2013

MATOKEO DARASA LA SABA YATANGAZWA

 
Serikali imetangaza matokeo ya darasa la saba ambapo watahiniwa wamefaulu 427, 606  kati ya watahiniwa 867,983 na watahiniwa 13 wamefutiwa matokeo ya mtihani kutokana na udanganyifu katika mtihani huo.

Akiongea na waandishi wa habari kaimu katibu mtendaji wa baraza la mitahani, Dk. Charles Msonde amesema wastani wa kufaulu umeongezeka kwa asilimia 19.89 ukilinganisha na mwaka jana(2012)  ambapo wastani wa kufaulu ulikuwa asilimia 30.72.

Msonde amesema jumla ya watainiwa walikuwa 867,983, waliopata daraja la A-C ni watahiniwa 427,606 ambapo ni wasichana 208,227 na wavulana 219,379, wakati watahiniwa waliopata daraja D ni 389,948, wavulana 166,010 na wasichana ni 223,9938 na daraja E ni watahiniwa 27,367 ambapo wavulani ni 13,425 na wasichana ni 13,942.

Ameongeza kuwa watahiniwa mwaka huu wamefaulu zaidi somo la Kiswahili kwa asilimia 60 na somo ambalo wamefaulu kwa kiwango cha chini ni somo la Hisabati ambapo wamefaulu kwa asilimia 28.62 ikilinganishwa na matokeao ya mwaka 2012.

Sambamba na hili, baraza la Mitihani Tanzania limefuta matokeo yote ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), 2013 ya watahiniwa 13 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

Aidha, amesema Baraza la Mitihani la Tanzania limewasilisha matokeo hayo kwenye Mamlaka husika ili zifanye uchaguzi wa watahiniwa wa kujiunga na elimu ya Sekondari.

Kwa upandu mwingine Msonde amesma Baraza la Mitihani la Tanzania kwa kujiridhisha na usahihi shaji kwa kutumia mfumo wa kompyuta (Optical mark Reader (OMR), Balaza lilitenga sampuli ya karatasi 20,795 ya majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka katika wilaya 48 za mikoa 9; Iringa , kagera, Shinyanga, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga ambazo zilisahihishwa kwa mkono na baadaye kufanya ulinganifu na usahihishaji wa OMR na kubaini kuwa mfumo wa kutumia kalamu kusahihisha ulikuwa na makosa ya kibinadamu kwa asilimia 1.2.

PICHA KUTOKA kIONGOZI BLOG
Mfumo wa kusahihisha Mitihani kwa kutumia mfumo wa kompyuta OMR ulianzishwa na Baraza la mitihani la Tanzania toka mwaka 2012 ambao umesaidia kupunguza idaidi ya washiriki wa usahihishaji kutoka washiriki zaidi ya 4000 hadi 302.

No comments: