Na Samwel Mbugi,
Iringa
Kukoseka elimu ya
mazingira miongoni mwa jamii ni moja ya sababu inayosabibisha kuongeza kwa
uharibifu wa mazingira nchini Tanzania.
Licha ya taasisi
zinazojishughulisha na utunzaji wa mazingira kuhimiza utunzaji wa mazingira
ikiwemo pamoja na kuanzisha kampeni ya kuzuia ukataji wa mistu pamoja na
kulima katika vyanzo vya maji mkoani, wananchi wengi mkoani Iringa hawana elimu
ya utunzaji wa mazingira hali iliyosababisha kampeni ya kupambana na uribifu
wa mazingira mkoani Iringa kutofanikiwa kwa kiwango cha kuridhisha.
Deodata Kayombo ni
mmoja wa viongozi wa wa Asasi rafiki kwa Mazingira Tanzania akizungumza na
wananchi mkoani Iringa alisisitiza elimu ya mazingira kuendelea kutolewa kwa
jiamii ili kuniusuru mazingira na kudhibiti athari zitokanazo na uharibifu wa
mazingira.
Uharibifu wa
mazingira mkoano Iringa umechangia kuongezeka kwa ukame na kupungua kwa vyanzo
vya maji mkoani humo hali iyosababisha kuongezeka kwa uhaba wa maji.
Kayombo alisema
tarafa ya Isimani amekumbwa na janga la ukame zaidi ya miaka thelathini kwa
sababu ya wananchi wa tarafa hiyo kukosa elimu ya mazingira.
Katika kuhakikiza azma ya kutunza
mazingira mkoani Iringa inaendelezwa, shirika hilo la Asasi Rafiki kwa
mazingira Tanzania limezindua mpango wa utunzaji mazingira ilikusaidiqa
kurudisha hadhi yake mazingira yaliyoathirika na ukame
Naye mkuu wa wilaya ya Iringa mjini,
Dr. Dr. Reticia warioba amewaasa wananchi
waliofikiwa na mpango huu kuhakikisha wanaonesha ushirikiano mzuri na asasi hiyo
kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Hata hivyo, biashara
ya mkaa imeonekana kushamiri mkoani Iringa hali iliyosababisha ukame na
uharibifu mkubwa wa mazingira.
Moja ya tanuru za mkaa ambayo imekuwa ni miongoni mwa biashara zinazompatia kipato mwananchi mkoani Iringa. |
Biashara ya mkaa mkoani Iringa imekuwa ni biashara kuu ambayo upatikanaji wa soko lake ni rahisi ukilinganisha na biashara ya mazao ya kilimo kama vile kahawa, alizeti na mpunga. |
Ukataji wa misitu holela huchangia uharibifu wa mazingira, ili kukamiliana na uharibifu wa mazingira serikali na asasi nyingine hazina budi kutoa elimu kwa jamii. (Picha zote ni kwa msaada wa tovuti) |