Na samwel
Mbughi, Mbeya
Katibu mkuu wa timu ya Tanzania Prison amezichimba
mkwara timu ya Mgambo JKT na timu ya Simba kuwa timu hizo zitegemee kichapo
kutoka kwao.
Akizungumza na mtandao huu katibu
wa timu ya Tanzania Prison SADICK JUMBE alisema kuwa wamejianda vyema kukipiga
na timu ya mgambo jkt, mchezo utakaotimua vumbi tarehe 02,
machi mwaka huu.
Jumbe aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwataka kuishangilia
timu hiyo kwa morali kubwa kwa kuwa wachezaji wameandaliwa kisaikolojia vizuri
na wapo tayari kuipitisha kichapo kwa timu yo yote watakayo kutana nao.
Sanjari na hilo, hakusita kuzungumzia
mchezo utakaotimua vumbi tarehe 8 Machi mwaka huu ukizikutanisha Tanzania Prison
dhidi ya timu ya simba katika uwanja wa sokoine jijini Mbeya.
Alisema
kuwa simba waende huku wakijua kuwa Tanzania Prison si timu ile ya zamania ni Tanzania Prison ni
timu ya sasa ambayo wachezaji wake wote wanacheza mfumo wa timu na wana morali
kubwa ya kushinda katika mechi zake ziliozosalia.
Aidha, Jumbe alisema kuwa mapungufu
yaliyokuwa yanaisabishia Tanzania Prison kufanya vibaya kipindi cha nyuma yametafutiwa
tiba yake na kocha wa timu hiyo.
Hata hivyo, Jumbe amewaasa waamuzi {marefa}
watakaochezesha mechi hizo kuzingatia sheria zote na kanuni zote za mpira wa
miguu ili kuepuka lawama.
Tanzania Prison msimu huu imeonekana kuanza
vizuri baada ya kutotambia na Wagosi wa Kaya Coastal Union na kisha kuwatandika
bakora mojo Mtibwa Sugar uwanja wa Manungu hatimaye kuwarusha kwata maafante
wanzao bila huruma JK Ruvu magoli 6 kwa yai, na baadaye kutoshana nguvu na timu
iliyopo kilele Azam FC yenye point 40 kwa magoli 2 kwa 2.
Timu ya Tanzania Prison ambayo hivi sasa imeanza kuonesha matumaini ya kusalia ligu kuu Tanzania Bara baada ya kuanza vizuri mzunguko wa pili. (Picha kwa msaada wa tovuti)Msimamo wa ligi kuu Tanzania bara
Msimamo wa ligi kuu Tanzania bara |
No comments:
Post a Comment