NGUVU YA HABARI

Friday, February 28, 2014

KUKOSEKANA KWA ELIMU YA MAZINGIRA KUNACHANGIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Na Samwel Mbugi, Iringa
Kukoseka elimu ya mazingira miongoni mwa jamii ni moja ya sababu inayosabibisha kuongeza kwa uharibifu wa mazingira nchini Tanzania.
Licha ya taasisi zinazojishughulisha na utunzaji wa mazingira kuhimiza utunzaji wa mazingira ikiwemo pamoja na kuanzisha kampeni ya kuzuia ukataji wa mistu pamoja na kulima katika vyanzo vya maji mkoani, wananchi wengi mkoani Iringa hawana elimu ya utunzaji wa mazingira hali iliyosababisha kampeni ya kupambana na uribifu wa mazingira mkoani Iringa kutofanikiwa kwa kiwango cha kuridhisha.
Deodata Kayombo ni mmoja wa viongozi wa wa Asasi rafiki kwa Mazingira Tanzania akizungumza na wananchi mkoani Iringa alisisitiza elimu ya mazingira kuendelea kutolewa kwa jiamii ili kuniusuru mazingira na kudhibiti athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira.
Uharibifu wa mazingira mkoano Iringa umechangia kuongezeka kwa ukame na kupungua kwa vyanzo vya maji mkoani humo hali iyosababisha kuongezeka kwa uhaba wa maji.
Kayombo alisema tarafa ya Isimani amekumbwa na janga la ukame zaidi ya miaka thelathini kwa sababu ya wananchi wa tarafa hiyo kukosa elimu ya mazingira.
Katika kuhakikiza azma ya kutunza mazingira mkoani Iringa inaendelezwa, shirika hilo la Asasi Rafiki kwa mazingira Tanzania limezindua mpango wa utunzaji mazingira ilikusaidiqa kurudisha hadhi yake mazingira yaliyoathirika na ukame
Naye mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Dr. Dr. Reticia warioba amewaasa wananchi waliofikiwa na mpango huu kuhakikisha wanaonesha ushirikiano mzuri na asasi hiyo kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Hata hivyo, biashara ya mkaa imeonekana kushamiri mkoani Iringa hali iliyosababisha ukame na uharibifu mkubwa wa mazingira.  
Moja ya tanuru za mkaa ambayo imekuwa ni miongoni mwa biashara zinazompatia kipato mwananchi mkoani Iringa.

Biashara ya mkaa mkoani Iringa imekuwa ni biashara kuu ambayo upatikanaji wa soko lake ni rahisi ukilinganisha na biashara ya mazao ya kilimo kama vile kahawa, alizeti na mpunga.

Biashara ya mkaa mkoani iringa inajulikana kwa jina maarufu mali nyeusi ikiwa tayari inasafirishwa kupelekwa sokoni. Kutokana kuwepo kwa soko la mkaa wananchi wengi vijiji husasan vijiana hujishughulisha na biashara hiyo

Ukataji wa misitu holela huchangia uharibifu wa mazingira, ili kukamiliana na uharibifu wa mazingira serikali na asasi nyingine hazina budi kutoa elimu kwa jamii.
(Picha zote ni kwa msaada wa tovuti)

No comments: