MABINGWA
wa Tanzania, Azam fc waaga rasmi mashindano ya kombe la Afrika Mashariki na
kati maarufu Kombe la Kagame kwa baada ya kunyukwa penati 4-3 dhidi ya El Merreik ya Sudan
katika mchezo wa robo fainali.
Mshindi
wa mchezo huo uliopigwa katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda, hadi
dakika 90 zinakamilika Azam FC 0 na El Merreikh 0.
Mikwaju
ya matuta ikaleta kilio kwa Azam baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizo kutotikisa
nyavu za ngoli la mwenzake (0-0).
Azam
FC walioneka kutokuwa na bahati ya kuchekelea nyavu za El Merreik baada ya washambuliaji
Kipre Herman Tchetche, John Bocco na Leonel Saint-Prexu kutotumia vema nafasi
walizopata.
Katika
hatua ya matuta Azam FM wanalambalamba walipata penati 3 ambazo zilifungwa na Aggrey
Morris, Didier Kavumbagu na Erasto Edward Nyoni, huku wachezaji wake Shomari
Salum Kapombe na Leonel Saint- Prexu ndiyo waliopeleka kilio Azam FC baada ya
kukosa penalti zao.
Katika
mchezo mwingine wa KCCA na ATLabara, Timu ya KCCA imeichalaza timu ya Atlabara
magoli 3 kwa 1, na kufanikiwa kutinga nusu fainali.
Kwa
matokeo hayo ya leo, Nusu fainali itazikutanisha timu mbili za Rwanda, Polisi
na APR na timu ya El Merreckh itachuana na timu ya KCCA.
No comments:
Post a Comment