Watanzania
wametakiwa wajibidishe kumcha mungu ili wapate malipo mema baadaye na kuacha tabia
kubaguana, kulumbana kwa sababu ya tofauti za imani yao ya dini.
Nasaha
hizo amezitoa pandre Emillius Haule wa kanisa la Anglikana la Mwenge wakati wa
ibada ya mazishi ya Bw. Dunstan Cuthbert Shaban aliyekuwa msajili wa kwanza wa
bodi ya taifa ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu - NBAA, aliyefariki jumanne wiki
hii.
Wakizungumza
katika maziko hayo mwenyekiti wa zamani wa bodi ya NBAA Dr Reginald Mengi, na
mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali Bw. Ludovick Utouh wamesema
wakati wa uhai wake marehemu Dunstan Shaban alikuwa mtu mwema, muadilifu
na mchapakazi hodari aliyejitoa kulitumikia taifa lake.
Aidha
katika salamu zao za rambirambi mkurugenzi wa NBAA Bw. Pius Maneno, na
mwenyekiti wa bodi ya kituo cha kutoa elimu kiitwacho the Universal Education
Centre Bw. Boko William Boko wamesema marehemu atakumbukwa kwa uzalendo wake na
mambo mengine mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake
No comments:
Post a Comment