Viongozi wa serikali wametakiwa katika kutekeleza vipaumbele
vya taifa badala ya kutumia muda huo kujipigia kampeni za urais mwaka 2015.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ametoa
kauli hiyo katika Kongamano la uhuru lililoandaliwa na Jumuiya ya Wataaluma wa
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDASA) ikiwa na kauli mbiu uhuru wetu na mstakabali wa miaka hamsini ijayo.
Butiku ametoa kauli hiyo akijibu hoja ya Naibu Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi naTeknolojia, January Makamba ambaye amewataka watanzania walizaliwa kabla ya mwaka
1961 wasigombee uongozi kwa kuwa wameshindwa kuiletea maendeleo bora nchini.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku |
Makamba amemhoji Butiku kuwa miaka yote waliyo kaa wamefanya
nini hadi tuwe na shule chache nchini.
Butiku amewashangaa viongozi wa serikali wanaozidi kulaumi
viongozi waliotangulia kuwa walifanya ni nini wakiwa madarakani badala ya
viongozi hao kujiuliza nini kifanyike katika kupambana na umasikini.
“Fanyeni kazi wenzako waone kwamba unafaa cheo cha urais, acheni
propaganda za kutafuta vyeo”, amesisitiza Butiku.
Amesema tiketi ya kuchaguliwa ni kufanya kazi kwa bidii na
kupunguza maneno yasiyosaidia kutekeleza mipango ya kazi za kimaendeleo ya
nchi.
Kauli hii imekuja mara baada ya baadhi ya viongozi wa
serikali kuacha wajibu wao katika kuwatumikia wananchi kwa kutumia muda mwingi
kujipigia kampeni za urais mwaka 2015, huku wapiga kura wao wakiendelea kupiga
miayo ya hali ngumu ya maisha.
No comments:
Post a Comment