Serikali imekiri kuwa Tanzania
ni nchi masikini, hivy o hatua za haraka zinahitajika ili kunusuru hali ngumu
ya maisha inayowakabili wananchi wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard
Membe, ametao kauli hiyo katika Mdahalo wa Uhuru ulioitishwa na Jumuiya ya
wanataluma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) katika ukumbi wa Nkame
Nkrumah.
“Ni kweli sisi ni masikini, lakini ni umasikini huu
tunauondoa wapi? Kuingia madarakani hakutaondoa umaskini bali kujenga viwanda,
kuboresha nishati na miundoo mbinu tufauondokana na umasikini,” alisisitiza
Membe.
Amewataka wasomi kushirikiana na serikali kufanya utafiti wa
kisayansi ili kupata mbinu zitakazo saidia kuikomboa Tanzania katika wimbi la umasiki.
Ameongeza kuwa wasomi ndiyo wanaotegewa katika kuhakikisha Tanzania
inatokomeza umasikini kwa kutoa elimu na kufanya tafiti mbalimbali zitakazo
isaidia serikali itumie katika shughuli nzima za uchumi na utawala wake.
Amesema idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kutoka watu
milioni kumi na tano mwaka 1961 Tanzania na sasa ina watu milioni 45 na kufikia
2013 tanzania itakuwa na watu milioni
65, hivyo utafiti wa haraka unahitajika ili kubaini njia mbadala zitakazo
saidia kuondoa umasikini nchini.
Ameongeza kuwa kutokana na umasikini Tanzania inakabiliwa na changamoto
za uhaba wa vifaa na dawa hospitali, miundo mbini mibovu, na ukosefu wa vifaa
vya kisasa vya kuchimbia madini pamoja na njaa.
Aidha, amesema serikali imejipanga kuboresha miundo mbinu ya
umeme wa kutosha ili kuweza kujenga viwanda ambavyo vitasaidia kuajiri wasomi
na vijana ili kupunguza hali ngumu ya maisha.
Lakini wasomi wamepinga vikali kauli hiyo kwa kusema kuwa Tanzania
ni nchi tajiri kwa kuwa ina maliasili nyingi ambazo zingetumiwa kwa manufaa ya
watanzania wenyewe zingefuta historia ya umasikini nchini.
Naye profesa Haji Semboja, amepinga kuwa Watanzania sio
masikini ila kinachosababisha umasikini Tanzania ni wananchi kukosa ya sera
taifa ya kujitegemea na kushindwa kuthibiti maliasili zilizopo kwa kuwaachia
wageni wamiliki maliasili ya watanzania.
Amesema madini ya Watanzania yanachimbwa na wageni na pindi
wanyeji wakichimba wanaitwa wavamizi na kuzuiliwa kuchimba madini yao, hali ambayo ina tetea
maslahi ya wageni na kuwagandamiza wenyeji.
Aidha, mwanasiasa wa CHADEMA, Esta Wasira amesema umasikini Tanzania umesababishwa na serikali mbovu ya
chama tawala ambayo imeshindwa kutetea masilahi ya raia wake badala yake
kujilimbikizia mali za umma
kwa manufaa yao
binafsi.
Ameongeza kuwa rushwa inayoendeshwa katika chaguzi
mbalimbali za chama tawala zinachochea uwepo wa umasikini nchini.
Amesema viongozi wanaoingia madarakani kwa njia ya rushwa
hawana lengo la kuwakomboa wananchi katika umasikini.
Naye mhariri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Martha Qoro, amesema
kukosekana kwa lugha rasmi ya kufundishia masomo yote shuleni, vyuoni na vyuo
vikuu ambayo itasaidia wanafunzi kupata elimu nzuri na hatimaye kulisaidia
taifa katika maendeleo.
Amesema wanafunzi wanahitimu kila mwaka lakini hawaleti
matunda kwa nchi hii ni kutokana na wanafunzi kufundishwa kwa lugha wasioielewa
na hivyo kuua vipaji na ubuni wa wanafunzi katika kuileta maendeleo ncho yao.
No comments:
Post a Comment