Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya kocha
wake mdenimark Kim Paulsen kesho kinashuka dimbani dhidi ya Mabingwa wa Afrika,
Zambia (Chipolopolo)au risasi za shaba, mchezo utakaopigwa uwanja wa taifa jijini
Dar es salaam kuanzia saa 10 jioni.
Nahadho wa kikosi cha Zambia na mchezaji bora wa
mwaka 2012 wa tuzo inayotolewa na BBC, Christopher Katongo ametamba kuibuka na
ushindi katika mchezo wa kesho, huku akijinasibu kutetea ubingwa wao wa afrika
pindi watakapo tua bondeni.
Katongo amesema wanatambua ugumu wa mashindano ya
2013 kwani kila timu inajiapanga kufanya vizuri lakini watajituma kufa na
kupona kuhakikisha wanatetea kombe walilopata mwaka huu februari nchini Gabon.
Wachezaji watakao kuwepo katika mchezo huo ni
Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy
Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa,
James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo
Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani
Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
MAKOCHA
Kuelekea katika
mechi ya kesho makocha mbalimbali wametoa tathmini yao kuhusiana na mchezo huo
wa kesho.
Mmoja wa
makocha hao ni kocha Keny Mwaisabula mzazi ambaye amesema mechi ya kesho ni
muhimu sana kwa taifa stars ukizingatia inakutana na mabingwa wa afrika ambao
watawapa changamoto nzuri vijana wa stars kuwakabili wamorocco mwakani kuwania
kufuzu fainali za kombe la dunia.
Mwaisabula
amesema stars inaweza kufanya vizuri japo watakutana na wachezaji bora wa Zambia
na wenye majina makubwa zaidi.
Naye kocha
wa mabingwa wa zamani wa kandanda Tanzania Afrian sports ya Tanga John Wiliam
maarufu kama Del Piero amesema Zambia na Tanzania hazitofautiana sana na miaka
ya nyuma tuliwazidi kiwango lakini sasa wanaonekana kujipanga vizuri kuliko
sisi.
Piero amesema
taifa stars kesho itapata ushindi kwani vijana wanaonekana kuwa makini na kuwa
na mabadiliko makubwa zaidi.
Mbali na
kuzungumzia mchezo huo, Del Piero amesema kesho timu yake itashuka uwanjani
kukabiliana na wapinzani wao wa jadi Makorora ya Tanga mjini, mchezo
utakaopigwa uwanja wa ccm mkwakwani mkoani Tanga.
Mechi
hiyo ambayo ni ya ligi ya mkoa wa Tanga iliahirishwa wiki iliypopita kutokana
na uwanja wa mKwakwani kuwa na matumizi mengine.
No comments:
Post a Comment