Na Samwel Mbugi, Mbeya
Mbeya City yashindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kubana mbavu na JKT Oljoro kutoka jijini Arusha katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mbeya City iliyoingia uwanjani kwa
kujiamini kuibuka na point tatu kibindoni ili kujiweka katika mazingira mazuri
ya kusaka ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara imejikuta dakika tisini zinamalizika
bila nyavu kucheka.
Kutokana na Mbeya City na JKT Oljoro kutoka suluhu, mashabiki wa Mbeya City wamechukizwa na matokeo hayo huku wakisema timu yao imecheza chini ya kiwango.
“Hii ilikuwa ni mechi ya kushinda kabisa tatizo timu yetu iliwadharau wapinzani wetu na wamecheza kama hawapo uwanjani vile,” alisema mmoja wa mashabiki wa Mbeya City
Hata Hivyo baadhi ya wachezaji walipohojiwa na mwandishi wa Nguvu Ya Habari walidai kuwa matokeo hayo yamesababishwa na kocha wao, JUMA MWAMBUSI ambaye anadaiwa kubadilisha mfumo wa uchezaji wa mpira ambao bado wachezaji hawajauzoea.
Kikosi cha Mbeya City kilicholazimishwa suluhu ya bila kufungana na timu ya JKT Oljoro ambayo ilidhaniwa kushuka daraja msimu huu. Kwa matokeo ya leo Mbeya City imejikusaji point 36. |
No comments:
Post a Comment