Mbarali,
Mbeya
Afisa
mtendaji wa kata ya Ihahi katika halmashauri a wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,
Costantino Tandika amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na viongozi ili
kuleta maendeleo ya kata hiyo.
Afisa
mtendaji Tandika amesema hayo wakati akizungumza na redio Ushindi katika kijiji
na kata ya Ihahi wilayani Mbarali katika mahojiano maalumu baada ya redio
Ushindi kutembelea vijiji kadhaa vya kata hiyo.
Amesema
ili jamii au taifa lo lote liendelea kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni
lazima kuwepo na mshikamano na ushirikiano baina ya viongozi na wananchi katika
shughuli za kimaendeleo.
Aidha
amesema ushirikiano walioupata kutoka katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri
ya wilaya ya mbarali umechangia kuinua maendeleo ya kijiji na kata yake ikiwemo
ujenzi wa shule ya msingi na sekondari, zahanati pamoja na ofisi ya Kata hiyo.
Hata
hivyo kauli ya mtendaji huyo wa kata imepingwa na wananchi wa Ihahi kuwa
maendeleo bado ni duni hususani huduma ya maji, shule na shughuli mbalimbali za
maendeleo ya kijiji na kata hiyo.
Aidha
wananchi hao wamesema viongozi wa kata hiyo kutanguliza mbele masilahi yao
kuchangia kurudisha nyuma maendeleo ya kata hiyo.
Baadhi
ya tuhuma kama za tatizo la maji na kijiji cha Ihahi kutoendelea kwa kiwango
kikubwa zikaelekezwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji Juma Mwahande na afisa
mtendaji wa kijiji hicho Abraham Shangwa aliyedai kuwa yeye ni mgeni kwani
ameanza kazi hapo mwaka jana.
Kwa
upande wake aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho kabla ya uchaguzi wa serikali za
mitaa disemba 14 mwaka huu Juma Mwahande anmekanusha tuhuma zilizotolewa dhidi
yake.
Wananchi ambao ni waajiri wakuu wa
viongozi wanaowachagua wanategemea vitu gani watafanyiwe na viongozi wao?
Kata ya Ihahi iliyopo Chimala wilayani
Mbarali ina jumla ya vijiji vitatu ambavyo ni Mwaluma, Ihahi na kijiji cha
Kibaoni ikiwa na wakazi wasiopungua elfu sita (6000) ambao huduma ya maji
wanategemea visima na mifereji inayopeleka maji katika mashamba ya wawekezaji
wilayani humo.
By
Josea Sinkala.
No comments:
Post a Comment