NGUVU YA HABARI

Saturday, September 17, 2016

KILIMO: WAKULIMA WA KAHAWA BADILISHENI AINA ZA MBEGU

Na Laudence Simkonda, Mbeya

Wakulima wa zao la Kahawa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wametakiwa kubadilisha mfumo wa uzalishaji wa zao hilo, kwa kuachana na kilimo cha zamani cha kutumia mbegu za asili na badala yake waanze kupandanda Mbegu za Kisasa.

Kwa mujibu wa Afisa ugani Lized Cope, Miongoni mwa mbegu zilizopendekezwa kutumiwa ni kahawa aina Compact inayozalishwa na taasisi ya utafiti wa mbegu Tanzania ambayo inadaiwa kuwa inaongeza thamani ya zao hilo.


Mojawapo ya mbegu za kahawa zinazodaiwa kustawi vizuri Wilayani Rungwe
Aidha amesema wakulima wengi wa Kahawa ndani ya wilaya hiyo, bado wanaendesha kilimo cha kizamani, kwa kutumia begu walizo rithi kutoka kwa mababu zao.

Kwa upande wao wakulima wa wilaya hiyo wamesema utitili wa kodi ya ushuru, ukosefu wa soko la uhakika na miundombinu mibovu ya barabara ni changamoto nyingine ambayo inawakatisha tamaa wakulima.

Hata hivyo, Meneja shirika la HNRS Richard Mbaga na Mwenyekiti Halmashauri ya Rungwe Ezekiel Mwakota wameyataka Mashirika binafasi kwa kushirikiana na Serikali ya wilaya kuhamasisha wakulima kuongeza juhudi za uzalishaji wa zao hilo.

Tuesday, December 8, 2015

Bodaboda Auawa Njombe



Dereva wa pikipiki Braison Mlonganile mkazi wa kijiji cha Nyumbo kata ya Ikuna mkoani Njombe ameuwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa mtoni.
Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi mkoani humo lina washikilia watu watatu akiwemo mwanamke mmoja wakihusishwa na tukio hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa mwili wa marehemu Braison Mlonganile umekutwa mtoni ukiwa na majeraha sehemu ya shingo yake.
Kamanda Mtafungwa alisema jeshi la polisi linatoa wito kwa raia kutojihusisha na matukio ya mauaji na kusema kuwa watii sheria bila Shuruti na kuwa watu wa kwanza kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

Wapateni Haki zao Watoto




Wazazi na walezi wametakiwa kuwapatia watoto wao haki za msingi ikiwemo elimu.
Selina Lyapinda ambaye ni mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Mbeya Women Organisation Prevention of HIV and AIDs alitoa rai hiyo wakati akizungumza na blogu hii Desemba 08 mwaka huu.
Alisema baadhi ya wazazi na walezi huwakatisha masomo watoto wao kwa kuwatumia kama vibarua nafuu wa kuinua uchumia wao, vitendo ambavyo huwanyima watoto haki zao za msingi ikiwemo haki ya elimu.
Mmoja wa wazazi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema watoto walio wengi hutafuta vibarua wenyewe ili wapate fedha za kujikimu pamoja na kulipa michango shuleni ambayo wazazi wao wameshindwa kuimudu kutokana na ugumu wa maisha.
Wakizungumza na blogu hii baadhi ya watoto ambao wamejiingiza katika vibarua vya kukata majani ya mifugo wamesema walikatisha masomo yao baada ya wazazi wao kukosa fedha za kuwasomeshea.

Kayombo Kabutali Amshangaa Rais Dk Mgufuli



Kaimu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Kayombo Kabutali amedai kuwa anamshangaa Rais John Magufuli kwa kupeleka sh. Bilioni 4 kwanye upanua wa barabara ya Mwenge jijini Dar es salaam huku baadhi ya Mikoa ikikabiliwa na baa la njaa.
Akizungumza na waandishi wa habari Kauli mjini Dodoma,
Kabutali alisema baadhi ya wananchi hawatanufaika na hatua hiyo kwa vile anaamini kuwa upanuzi wa barabara hiyo hautasaidia kutekeleza kipengele cha msingi cha haki za binadamu.
Aidha alisema kwa utaratibu huo, baadhi ya makundi ya wananchi hawatamuelewa hata kama utendaji kazi wake unakubalika.
Kibutali, alisema fedha hizo zingepelekwa mkoa wa Simiyu zisaidie familia zilizokumbwa na baa la njaa hasa akinamama na watoto wadogo ambao wamekosa msaada wa chakula baada ya wanaume kutelekeza familia zao.
Alisema rais alitakiwa atoe kipaumbele kwa baadhi ya Mikoa ambayo ina uhaba wa chakula ukiwemo Mkoa wa Dodoma.