Wazazi na walezi wametakiwa kuwapatia watoto wao
haki za msingi ikiwemo elimu.
Selina Lyapinda ambaye ni mkurugenzi wa shirika
lisilo la kiserikali Mbeya Women Organisation Prevention of HIV and AIDs alitoa
rai hiyo wakati akizungumza na blogu hii Desemba 08 mwaka huu.
Alisema baadhi ya wazazi na walezi huwakatisha
masomo watoto wao kwa kuwatumia kama vibarua nafuu wa kuinua uchumia wao,
vitendo ambavyo huwanyima watoto haki zao za msingi ikiwemo haki ya elimu.
Mmoja wa wazazi ambaye hakutaka jina lake litajwe
alisema watoto walio wengi hutafuta vibarua wenyewe ili wapate fedha za
kujikimu pamoja na kulipa michango shuleni ambayo wazazi wao wameshindwa
kuimudu kutokana na ugumu wa maisha.
Wakizungumza na blogu hii baadhi ya watoto ambao wamejiingiza
katika vibarua vya kukata majani ya mifugo wamesema walikatisha masomo yao baada
ya wazazi wao kukosa fedha za kuwasomeshea.
No comments:
Post a Comment