Kaimu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Ukombozi wa
Umma (CHAUMA), Kayombo Kabutali amedai kuwa anamshangaa Rais John Magufuli kwa
kupeleka sh. Bilioni 4 kwanye upanua wa barabara ya Mwenge jijini Dar es salaam
huku baadhi ya Mikoa ikikabiliwa na baa la njaa.
Akizungumza na waandishi wa habari Kauli mjini Dodoma,
Kabutali alisema baadhi ya wananchi hawatanufaika na hatua hiyo kwa vile anaamini kuwa upanuzi wa barabara hiyo hautasaidia kutekeleza kipengele cha msingi cha haki za binadamu.
Aidha alisema kwa utaratibu huo, baadhi ya makundi ya wananchi hawatamuelewa hata kama utendaji kazi wake unakubalika.
Kibutali, alisema fedha hizo zingepelekwa mkoa wa Simiyu zisaidie familia zilizokumbwa na baa la njaa hasa akinamama na watoto wadogo ambao wamekosa msaada wa chakula baada ya wanaume kutelekeza familia zao.
Alisema rais alitakiwa atoe kipaumbele kwa baadhi ya Mikoa ambayo ina uhaba wa chakula ukiwemo Mkoa wa Dodoma.

No comments:
Post a Comment