Suala la wanafunzi kuripoti mapema chuoni kwa ajili ya masomo
limekuwa sugu kutokana na sababu mbalimbali zinazowafanya wanafunzi kuchelewa
kuripoti huku wahadhiri wakiwasubiri madarasani mwao.
akifanya mahojiano na mwandishi wa The Hill Observer, kaimu
mkuu wa shule, Maico Andindilile alikiri tatizo kuwa sugu huku akisema hakuna
njia yeyote ya kulimaliza tatitizo hilo isipokuwa wanafunzi wenyewe wahakishe
kuripoti chuo.
Wanafunzi wa Shahada ya Uandishi wa Habari wakiwa katika
picha ya pamoja na Mhadhiri wa SJMC- UDSM, Mr. Abdallah Katunzi (aliyevaa suti
nyeusi na miwani) baada ya kazi nzito kukamilisha ya kuandaa gazeti la Jicho
Huru ambalo wamelianzisha ili kuinua uweledi wa tasnia ya habari. Picha na
Ndaga Mwaipopo
“Wanafunzi wengi wanategemea mikopo, hivyo husubiri kwanza
wasaini na wapewe fedha zao ili waanze mchakato wa usajili. Hivyo inakuwa ngumu
kama bado hawajapewa fedha zao na shuleni hawawezi kusoma kama hawajafanya
usajili”, alisema Dk Andindilile.
Aliongeza kuwa wiki ya masomo iliyopotea haitafidiwa kwa
namna yeyote kwa kuwa si kosa la uongozi wa chuo kwa wanafunzi kuchelewa na
chuo kinafanya shughuli zake kwa kuzingatia ratiba waliyojipangia ya mwaka
mzima na kwa kufanya hivyo ni kuharibu ratiba nzima ya chuo.
“Hatuwezi kufidia wiki moja ya masomo iliyopotea kwa kuwa si
utaratibu wa chuo, labda mwalimu mwenyewe wa somo husika aamue kufidia somo
lake la wiki iliyopotea kwa kutumia vipindi vya ziada ndani ya siku za masomo
kwa kukubaliana na wanafunzi wake lakini asifidie siku za wikiendi ataharibu
ratiba za wanafunzi wanao Sali siku hizo”, alisisitiza Dk. Andindilile.
Aidha alitoa ushauri kwa wanafunzi wasiotegemea mikopo
kuripoti mapema chuoni na wanafunzi wanaotegemea mikopo nao watafute fedha za
kuanzia ili kuepuka kuchelewa kuanza masomo kwa manufaa yao kwa kuwa kupoteza
wiki ya masomo ni hasara kwa wanafunzi wenyewe na si kwa mwalimu.
Naye, Mwenyekiti wa serikali ya wanfunzi ya Shule kuu ya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma DARUSO(SJMC), Michael Christopher
alisema tatizo la wanafunzi kuchelewa kuripoti limekuwa sugu kutokana na
wanafunzi wenyewe kutokuwa na moyo wa kupenda kuwahi na kushauriana vibaya na
wenzao kwa visingizio vya kusema wiki ya kwanza ni wiki ya usajili na
kuwaonesha mazingira mwaka wa kwanza jambo ambalo alidai kuwa si la kweli.
“Waache kushauriana vibaya, masomo yanaanza mara tu chuo
kinapofungua. Kama ilivyokuwa wiki hiyo ya masomo iliyopotea ambayo walimu
waliingia madarasani lakini walikosa wanafunzi wa kuwafundisha”, alisema Mr.
Michael.
“Mfano mzuri, mwalimu Malima aliingia darasa la mwaka wa pili
Jumanne akatoa jaribio ‘test’, wanafunzi waliokuwepo walifanya na wengi
walikosa jaribio ‘test’ hiyo, vile vile mwalimu Kaijanangoma aliingia
kufundisha darasa la mwaka wa tatu akawakuta wanafunzi wachache sana hali
iliyosababisha ahahirishe hadi wiki iliyofuata ili awasubiri wanafunzi wafike
angalau nusu ya darasa”, aliongeza Mr. Michael.
Aliongeza kuwa wanafunzi wengi wanaotegemea mkopo wanachelewa
kuanza masomo kutokana na kusubiri wapewe hela zao iliwaweze kulipa ada ili
wasajiliwe na bila kufanya hivyo chuo hakiwa tambui.
“Ni vigumu kwa mwanafunzi anayetegemea mkopo atoke mkoani aje
chuoni asaini halafu asubiri fedha zake wiki
moja wakati hana fedha za kujikimu na hapati msaada wowote, hapa lazima
tu atachelewa kuripoti hadi apewe fedha zake”, alisisitiza Mr. Michael
Aidha alisema uongozi wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) unaendelea
kufanya mipango ya mawasiliano na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
na uongozi wa chuo kupata suluhisho la kuwapa fedha mapema wanafunzi angalau
kabla ya wiki moja chuo kufungua.
Nao baadhi ya wanafunzi walipoulizwa kuhusiana na suala hili
walidai kuwa tatizo kubwa ni vitendo vya ucheleweshwaji fedha zao na bodi Ya
mikopo husababisha kukosa fedha ya kujikimu pamoja na nauli.
No comments:
Post a Comment