Akina mama mkoani Iringa katika Jimbo la Kalenga wakishangilia baada ya Godfrey Mgimwa kuibuka mshindi wa ubunge jimboni hapo |
Uchaguzi
wa jimbo la kalenga uwe fundisho kwa chaguzi zijazo kwa vyama vya siasa na
vyombo vya dola vinavyohusika kulianda Amani na usalama wa nchi pamoja na raia
wake.
Licha
ya uchaguzi wa jimbo la Kalenga kumalizika na Godfrey Mgimwa (CCM) kuibuka
kidedea bado umeacha kovu lisilotibika haraka miongoni mwa walioumizwa kipindi
cha kampeni za uchaguzi huo.
Katika
kampeni hizo CHADEMA na CCM vilikuwa vikituhumiana kwa kuwatumia vijana katika
matukio ya kiuhalifu kama vile kuwakamata viongozi wa vyama hivyo na kuwapiga
na hata kuwateka viongozi hao.
CCM
waliwatuhumu wafuasi wa CHADEMA kupiga na kumuumiza kiongozi wa CCM na dereva
wa Naibu Waziri wa Uchumi Mwigulu Nchemba wakati CHADEMA wakiwatuhumu wafuasi
wa CCM kwa kumpiga mchungaji wa kanisa la Orthodox, na kumpiga mbunge wa viti
maalum wa CHADEMA Rose kwa madai alikuwa anatoa rushwa kwa wapiga kura.
Kasoro
zote zilizojitokeza kipindi cha kampeni hadi uchaguzi serikali na vyama vya
siasa havina budi kutafuta suluhu ya kutatua kasoro hizo ikiwemo kuwafundisha
vijana wao namna ya kufanya kampeni za Amani kwa kutoa sera za kuwashawishi
wananchi wamkubali mgombea badala ya kushindana kwa virungu na mapanga.
Matukio
haya yote kama yatafumbiwa macho hakika yataliingiza taifa katika machafuko ya kisiasa yasiyo na
tija yoyote kwa taifa hili.
Kukomaa
kwa Demokrasia si kushindana kwa kupigana bali ni kushindana kwa sera na pindi
mtu anaposhindwa katika uchaguzi baada ya wananchi kuamua kumpa kura mtu
mwingine, aliyeshindwa basi anakubaliana na matokeo na kumpongeza aliyepita.
Sasa
baada ya wanakalenga kumchugua Godfrey Mgimwa kuwa mbunge wao, mbunge huyo hana
budi kuondoa tofauti zao zote na wanachama wa vyama vya upinzania na
kuwatumikia wananchi wake kwa kuhakikisha ahadi zilizo ahidi katika kipindi
hiki kifupi cha uchaguzi anazitekeleza kwa muda mwafaka ilikujiwekea mazingira
ya kukubalika na wananchi wa kalenga.
Wanakalenga
hawakuhitaji na wala hawakumchagua kwa ngonjera za ahadi bali wamempa fursa
hiyo ya kuwatumikia wananchi hao baada ya kumwona ametambua matatizo
wanayokabiliwa nayo ambayo mbunge huyo atayatatua katika kipindi hiki kifupi
cha mwaka mmoja.
Hata
hivyo si dhambi kwa mbunge mteule Mgimwa akatimiza baadhi ya malengo ambayo
yaliaachwa na marehemu Williamu Mgimwa badala ya kuongeza ahadi nyingi
zisizotekelezeka kwa wanakalenmga kwa lengo tu aonekana ana ahadi na malengo
mazuri kwa wananchi wa Kalenga.
Aidha,
katika kampeni wanafunzi ama watoto walichukuliwa kama mfano wa kuonesha namna
gani serikali ya chama tawala inavyoshindwa kuwasaidia wananchi hata wanafunzi
katika kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu ya jamii.
Ni
wazi sasa aliyepita atahakikisha pia wanafunzi waliooneshwa kama mfano wa
wanafunzi wanaotoka katika familia masikini wanasaidie na wanapata elimu sawa
na watoto wa vigogo badala ya kuwaacha watoto katika mazingira yale yale ambayo
hayaoneshi utofauti wo wote wa chama hicho kugundua kuwa watoto hao wanatoka katika
familia masikini.
Hata
hivyo kuna haja ya kuangalia upya sheria ya vyama vya siasa ili ifanyiwe
mabadiliko kutokana na sheria hiyo kutokuwa na kikomo cha idadi ya vyama vya
siasa vinavyotakiwa kusajiliwa nchini.
Kutokana
na sheria hiyo kukosa meno ya imesababisha utitiri wa vyama vingi vya siasa
ambavyo vinaonekana kuanzishwa kwa malengo ya kupata ruzuku ambayo inaingia
mifukoni mwa watu wachache.
Ruzuku
zinazotolewa kwa vyama vya siasa ni fedha za wananchi ambazo zingeweza
kuwasaidia wananchi katika mambo mengine ya msingi kwa jamii.
Uwingi
wa vyama vingi nchini Tanzania haumanishi kukomaa kwa Demokrasia kwa kuwa nchi
zilizoendelea kama marekani ina vyama viwili tu na bado ni nchi iliyokomaa
kidemokrasia.
Wapiga kura katika Jimbo la Kalenga Mkoani Iringa wakiwa tayari kwa kupiga kura kumchagua mgombea wapendaye baada ya kampeni za kujinadi wagombea hao kuwashawishi wananchi hao na kuamua kwa hiari yao nani wape kura zao. (Picha kwa msaada wa Michuzi blogu) |
No comments:
Post a Comment