Kanisa
la EAGT Samaria Mikocheni A, jijini Dar es Salaaam limetangaza siku kumi za
maombi ya kufunga kwa ajili ya kuombea bunge la Katiba, Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwakani 2015.
Askofu
msaidizi wa Jimbo la Kinondoni na Mchungaji
wa kanisa la EAGT Samaria Mikocheni ‘A’, Filipo Phiri alitangaza maombi
hayo wakati akitoe neno la Mungu kwa waamini wake Machi 2, mwaka huu na
kuwataka waumini wa kanisa hilo kujitoa mhanga katika kuombea mambo hayo muhimu
kwa taifa la Tanzania.
Pamoja
na hayo, Mchungaji Phiri alisema anashangazwa na namna bunge la Katiba lilivyoanza
kwa kutanguliza masilahi ya vyama vyao huku maoni yaliyotolewa na wananchi likitaka
kuyaacha kwa kutoa maelezo yanayokinzana
na tume ya Warioba kwa kudai kuwa linaweza kubadilisha kabisa mapendekezo yote
yaliyokusanywa na tume.
“Rasimu
ya Katiba hii ikipitishwa itasaidia kukomesha masuala ya ufisadi, wizi wa mali
za umma pamoja na uzembe wa viongozi wetu kwa kuwa inawapa mamlaka wananchi
kumtoa kiongozi wao au mbunge wao kama hafanyi vizuri,” alisema mchungaji
Phiri.
Aliongeza
kuwa kama rasimu hiyo itapishwa itasaidie pia kutatua migororo ya kisiasa
nchini inayosabishwa na tume ya chaguzi kutokuwa huru kwa sababu rasimu
inapendekeza tume huru ya uchaguzi.
Aidha,
mchungaji Phiri aliwaasa wakristo kuachana na dhana potofu kuwa kujihusisha na
siasa ni dhambi na kuwataka wao wawe wa kwanza kujiunga na vyama wanavyovipenda
na kugombea ngazi mbaliombali za uongozi.
“Msipochukua
fomu za kuogombea katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa
madiwani, wabunge na rais, mnataka mtawaliwe na nani?
“Hakuna
maandiko yoyote kwenye Biblia Takatifu yanayomzuia mkristo kujihusisha na
siasa, au kutogombea ila ninyi wenyewe mkikaa makundi makundi mnanyidanganya hivyo
kuwa biblia inakataa kujihusisha na siasa, chukueni fomu gombeeni,” alisisitiza
mchungaji Phiri.
Mchungaji
Phiri aliwaambia waumini wake kuwa waamini kuwa katika maombi hayo ya siku kumi
Mungu atakwenda kuwatendea Watanzania kwa kuwapatia Katiba nzuri inayotokana na
wananchi, kuwa na chaguzi za huru na za Amani bila umwagaji wa damu.
“Tuhakikishe
katika maombi yetu ya siku kumi tunawaombea wajumbe wa Katiba, uchaguzi wa
serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwakani.
“Tuombee
tu kwa imani na Mungu atakwenda kuwatendea watanzania sawasawa na vile
tulivyoomba na hakika Mungu atawasaidia wajumbe wetu huko Dodoma,” alisema
mchungaji Phiri.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa CASFETA-TAYOMI (AGM) wakiwa katika vikao vya vikundi kujadili mambo mbalimbali kabla ya kuwasilisha ripoti ya maendeleo ya utekelezaji wa mipango na mikakati kwa kamati kuu na kufanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya taifa mjini Dodoma uliofanyika mwaka 2012, {Picha imechukuliwa mabakta} |
No comments:
Post a Comment