Na Samwel Mbugi, Mbeya.
Wadau na wapenzi wa soka jijini Mbeya wametoa
maoni yao kuhusiana na msimu huu wa mashindano ya ligi kuu Tanzania Bara
msimu wa 2013/2014 wakilinganisha na mashindano ya msimu wa mwaka jana
2012/2013.
Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati
tofauti walisema kuwa msimu huu ni mgumu sana ikilinganishwa na miaka
mingi iliyopita timu zilizo kuwa zinaonyesha upinzani mkubwa dhidi ya Young
Africans Sports Club (Yanga) na Simba Sports Club zilikuwa chache lakini msimu huu unaonesha
kila timu imejipanga kuleta ushindani mkali bila kuogopa vilabu vikongwe.
Pia walisema
kuwa mwaka huu haitabiriki haraka timu itakayochukua ubingwa kwani kila
timu inaonekana kujianda vyema kitu ambacho kimeleta changamoto kwa timu
kubwa zilizozoea kuchukua ubingwa wa mashindano ya ligi kuu Tanzania Bara.
Mpaka sasa Timu za Azam FC, Young Africans
Sports Club na Mbeya City zina nafasi kila moja ya kutwaa ubingwa mwaka huu.
Bingwa mtetesi Young Africans Sports Club yupo
nyuma kwa pointi 4 dhidi ya makamu bingwa Azam FC mwenye pointi 47 na akiwa na
mechi moja mkononi, huku Mbeya City akiwa na Pointi 42.
Wachezaji wa Young Africans Sports Club wakicheza kiduku bada ya kufunga goli la Kuongoza dhidi ya Azam FC (Picha Kwa Msaada wa Full Shangwe) |
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli baada ya kurudisha goli dhidi ya Yanga mechi ambayo iliisha kwa timu hizo kufungana 1:1.(Picha Kwa Msaada wa Full Shangwe) |
Sambamba na hayo wengi wao walitoa ponge
kwa timu ya Mbeya City kwa kuonyesha upinzani mkubwa licha ya kuwa ni mara ya
kwanza kucheza mashindano hayo ya ligi kuu Tanzania Bara.
Wamezitaka timu za ligi daraja la kwanza kuiga
mfano kwa timu ya Mbeya city.
Wachezaji wa Mbeya City pamoja na mashabiki wao wakishangilia ushindi wa 2:0 dhidi ya Ruvu Stars. (Picha Kwa Msaada wa Full Shangwe) |
No comments:
Post a Comment