Na Faraja Muwanje, MBEYA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu
25 Raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Mbeya Ahmed Msangi
amesema raia hao wamekamatwa wakiwa wamefichwa kwenye nyumba ya mwananchi
ambaye ni mkazi wa uyole.
Wahamiaji hao wanadaiwa kuingia Nchi bila vibali, ikiwa
ni siku tatu zimepita tangu watu wengine 75 walipokamatwa mjini Mbeya
wakijaribu kuvuka mpaka kuelekea Nchi za
Kusini.
Idadi ya watu wanaoingia nchini wakielekea Nchi za
kusini imezidi kuongezeka hali inayotishia usalama na amani kwa maeneo yaliyokuwa
pembezoni ikiwemo wilaya ya Ileje na Momba Mkoani Mbeya.
Kamanda
Ahmedi Msangi amesema unahitajika uzalendo katika kudhibiti na kukomesha
misafara ya watu wanaoingia Nchini bila vibali.
No comments:
Post a Comment