Na
Betty Gilbert, MBEYA
Baadhi ya wananchi mkoani mbeya wametoa maoni yao juu ya tamko la vyama vinavyounda umoja wa katiba ya
wananchi (UKAWA) la kutoshiriki katika zoezi la kuipigia kura katiba
inayopendekezwa ifikapo aprili 30 mwaka huu.
Wakizungumza na Nguvu ya Habri february 26 mwaka
huu baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa umoja huo uko sahihi kususia zoezi
hilo wakidai kuwa maoni ya walio wengi yamepuuzwa.
Hata hivyo wameongeza kuwa mbali na kupuuzwa kwa
maoni ya wananchi, wamesema hata katiba ya kwanza hawaifahamu, hivyo kujua
marekebisho yaliyofanywa katika katiba mpya itakuwa ni vigumu hata kama wataisoma.
Nao baadhi ya viongozi wa ukawa wamesema katiba
inayopendekezwa imeacha asilimia tisini ya maoni yaliyopendekezwa na wanachi, hivyo
wamedai kuwa hawaoni haja ya ukawa pamoja na wananchi wenye uzalendo na nchi
yao kuipigia kura ya ndiyo katiba hiyo.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa upande wa chama
cha mapinduzi (ccm), wamesema
kuwa kiongozi yeyote lazima afuate kanuni na sheria na siyo kufanya maamuzi
yake binafsi bila kufikiria mustakabali wa taifa na kudai kuwa hakuna sababu ya ukawa kutoshiriki
kupiga kura.
No comments:
Post a Comment