Na Atu
Mbotwa, MBEYA
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya wamewalalamikia
viongozi wa Serikali za mitaa kwa kutoa maamuzi kuhusu mipango ya maendeleo
bila kuwashirikisha wananchi.
Wamesema hayo Februari 26, mwaka huu kwa nyakati
tofauti wakati wakizungumza na Nguvu ya Habari ambapo wamesema kuwa migogoro mingi
hujitokeza kutokana na viongozi kufanya maamuzi yanayogusa mustakabali wa
wananchi bila kuzingatia maoni ya wananchi husika.
Kwa upande wao wenyeviti wa mitaa ya Sokoni na
Mponja wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo kwa baadhi ya viongozi, jambo ambalo
wameeleza kuwa ni kinyume cha Sheria na maadili ya uongozi.
Wamesema kuwa, Sheria inawataka viongozi wa mitaa
kuandaa angalau mikutano sita kwa mwaka kwa ajili ya kujadili na wananchi kuhusu
mipango ya mtaa husika.
Kwa
Mujibu wa Katiba, Wajibu na Haki ya kila Mwananchi katika Kijiji ni Kuhudhuria
mikutano yote katika kitongoji, kijiji na mtaa na kuhakikisha kuwa mikutano
inafanyika kila baada ya muda uliopangwa, Kulinda mali, rasilimali za umma na
kupambana na kila aina ya uovu ikiwemo ubadhirifu, wizi, rushwa na mengineyo.
Pia,
Kumwondoa kiongozi au viongozi wasiowajibika kwa kumpigia kura ya hapana, Kujenga
na kuimarisha mshikamano uliopo katika jamii yake, Kushiriki kupanga, kusimamia
na kuthathimini na kuhoji matokeo ya miradi
yote katika kitongoji, kijiji na mtaa, Kushiriki katika
kupiga na kupigiwa kura kugombea nafasi za uongozi na Kuheshimu kiongozi au
viongozi wake.
Hivyo
Kwa mujibu wa Katiba ni kosa kwa Kiongozi wa Serikali ya Mtaa, Kijiji na
Kitongoji kufanya shughuli za mtaa bila kuwashirikisha wananchi wa mtaa husika.
No comments:
Post a Comment