Na
Petro Kalago, MBEYA
Serikali
imewataka viongozi wa dini kuwa makini na wanasiasa ambao hukimbilia kutoa
misaada makanisani wakati uchaguzi unapokaribia kwa ajili ya kujitafuatia
umaarufu.
Akihutubia katika kongamano lililowakutanisha
viongozi wa dini ya kikristo na kiislam februari 26 mwaka huu Mkurugenzi wa
taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya Felix Wandwe,
amesema viongozi wa dini wawe makini kwa kipindi hiki cha uchaguzi kwani baadhi
ya watu hujipendekeza kwa kutoa misaada bila sababu.
Aidha, amesema kuwa Mwaka huu watanzania wana
mambo makuu matatu wanayotarajia kuyafanya ambayo ni Uandikishaji wa wapiga
kura katika daftari la kudumu la wapiga kura, kuipigia kura ya maoni katiba
inayopendekezwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Naye Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa
Mbeya Samora Saranga akihutubia katika kongamano hilo kwa niaba ya kamanda wa
jeshi polisi mkoa Ahmed Msangi amesema kuwa matukio ya uharifu katika Mkoa wa
Mbeya yameendelea kuongezeka kutoka Mwaka 2013-2014 kwa kiasi kikubwa na kusema kuwa viongozi wa
dini wana nafasi kubwa katika kukemea maovu yanayojitokeza katika jamii.
Sambamba na hayo wametoa wito kwa jamii kujitokeza
kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
pia kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi
oktoba mwaka huu bila kathiri Amani ya Taifa.
No comments:
Post a Comment