Afisa mtendaji wa mtaa wa Hayanga kata ya Ilomba
jijini Mbeya Maria Mwaiswelo ameitaka jamii kuwa na mwamko mpya wa kutoa
taarifa za kuwepo kwa matukio yanayotokea katika maeneo yao kwenye vyombo
vinavyohusika kwa hatua zaidi za kisheria.
Mwaiswelo ametoa rai hiyo February 27 mwaka huu
alipotembelewa na Nguvu Ya Habari ofisini kwake kufuatia kuwepo kwa tukio la mtu
mmoja kutuhumiwa kuwabaka watoto kadhaa katika mtaa huo bila kitendo hicho
kufikishwa katika ngazi zinazohusika.
Maria amesema ofisi yake haina taarifa yoyote ya
kuwepo kwa mtu aliyewabaka watoto wanaokadiliwa kuwa sita katika mtaa huo hivyo
amesema hawezi kuzungumzia zaidi tukio hilo huku akiitaka jamii kutoa taarifa
juu ya kuwepo kwa vitendo kama hivyo badala ya kutaka kumaliza masuala hayo
kindugu.
Mmoja wa watoto hao mwenye umri wa miaka saba (7)
na mwanafunzi wa shule ya msingi Ikulu wanaodaiwa kubakwa na kuchezewa na
mtuhumiwa anayeelezwa kutenda vitendo hivyo kwa nyakati tofauti ameiambia
Nguvu ya Habari kuwa alikuwa akiitwa na mtuhumiwa na kuanza kumfanyia vitendo
hivyo akimlaghai kwa kumpatia fedha kiasi cha shilingi hamsini.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo (Jina limehifadhiwa)
akizungumzia tukio hilo Amesema baada ya kupata taarifa juu ya mwanae kutendewa
kitendo hicho alimjulisha mume wake kwa kuwa hakuwepo nyumbani ndipo wakaenda
kutoa taarifa kwa balozi wa mtaa huo na kwamba hatua zilikuwa bado hazijaanza
kuchukuliwa.
Amedai kusikitishwa na kitendo hicho ambapo
ameiomba serikali na vyombo vinavyohusika kumsaidia kwa ajili ya hatua zaidi za
kisheria ikiwemo kukamatwa kwa mtuhumiwa na kwamba wanafanya taratibu kwa ajili
ya kumpeleka mtoto wao hospitali kwa uchunguzi zaidi wa kiafya.
Mwenyekiti wa mtaa huo Godliving Paul Koka amesema
taarifa rasmi za tukio hilo hajizamfikia na kuahidi kushirikiana na viongozi
wengine pamoja na wananchi ili kuhakikisha mtuhumiwa anachukuliwa hatua za
kisheria.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema vitendo
kama hivyo havitakiwi kufumbiwa macho ambapo mtuhumiwa huyo aliyetajwa kwa jina
la Lukas Mwangono amekuwa akifanya vitendo hivyo kwa muda mrefu ambavyo
vimekuwa kero kwa ndugu na majirani wa mtaa huo.
Aidha wamesema mtuhumiwa amekuwa na kawaida ya
kuwachezea watoto wa ndugu zake hivyo kutotafuta hatua zaidi za ufumbuzi bali
wamekuwa wakiyamaliza masuala hayo kifamilia tofauti na awamu hii ambapo baada
ya kikao cha baadhi ya wananchi kilichofanyika February 26 mwaka huu mtuhumiwa
alikimbia na haijulikani aliko.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo Lukas Mwangomo alipopigiwa
simu kujibu tuhuma hizo amegoma kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Kwa upande wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
Kupitia Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Samora Saranga amwesema Jeshi la
Polisi haliwezi kuchukua hatua zozote kwakuwa tukio hilo halijaripotiwa Polisi,
hivyo kuwataka wazazi wa watoto waliokumbwa na mkasa huo kutoa taarifa katika
vyombo vinavyohusika.
No comments:
Post a Comment