Na
Faraja Muwanje, MBEYA
Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mkoa
wa Mbeya kimesema hakitaruhusu watu wanaotaka kutangaza nia katika majimbo
ambayo yanaongozwa na chama hicho mpaka pale bunge litakapovunjwa rasmi kwa ajili
ya uchaguzi kutokana na sheria za chama hicho.
akizungumza
na blogu ya Nguvu ya Habari kwa njia ya simu machi 13 mwaka huu, Mwenyekiti wa chama hicho
wilaya ya Mbeya David John Mwambigija amesema chama hakiwezi kuruhusu watu
kutoka ndani ya chama kutangaza nia ili kuepuka wabunge na madiwani walioko
madarakani kufanya vibaya kwa muda uliosalia.
Aidha Mwambigija amekiri kuwepo kwa watangaza nia
wengine nje ya jimbo la Mbeya akiwemo yeye mwenyewe na kuelezea baadhi ya sifa
za mtu anayetaka kutangaza nia ndani ya chadema ikiwa ni pamoja kuandika barua
na kupeleka katika jimbo analotaka kugombea.
Hata hivyo Mwambigija alipoulizwa utaratibu wa
watangaza nia kupitia muundo wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA amesema wanaangalia chama kimojawapo ndani ya
UKAWA kinachokubalika eneo fulanina ndicho kitakacho simamisha mgombea.
Pia kituo hiki kimezungumza na katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbeya mjini
Kulwa Millonge ambaye amesema kwa upande wa chama chake utaratibu wa kutangaza
nia bado haujatangazwa katika chama hicho, hivyo wanasubiri maelekezo kutoka
makao makuu.
Uchaguzi mkuu kuchagua rais, wabunge na madiwani utafanyika oktoba mwaka huu,ambapo
viongozi wenye nia ya kuwania katika ngazi mbalimbali za uongozi wanatumia muda
uliobaki kujinadi kwa wananchi wao ili kupigiwa kura wakati ukifika.
No comments:
Post a Comment