JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14.03.2015.
·
WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAJARIBU
KUFANYA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWA MFANYABIASHARA WA MADINI AINA YA
DHAHABU WILAYANI CHUNYA.
·
WALINZI WAWILI WA CITY PUB JIJINI MBEYA
WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA NA KUMJERUHI
MFANYABIASHARA MMOJA MKAZI WA ISANGA.
·
MWANAMKE MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA
MTOTO CHOONI MWENYE UMRI WA SIKU MOJA.
·
WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI NUSU LITA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAKIWA NA VIPANDE SITA VYA MENO YA TEMBO.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AITWAE
ROBERT MBUKWA (50) MFANYABIASHARA YA MADINI AINA YA DHAHABU NA MKAZI WA MIANZINI WILAYANI
CHUNYA ALIVAMIWA NA VIJANA WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAKIWA NA
SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA SHOT GUN 12 BORE
YENYE NAMBA 64943 ILIYOTENGENEZWA
KATIKA KIWANDA CHA WEMBLEY @ SCOTT LTD
KILICHOPO BIRMINGHAM ENGLAND NA KUFYATUA RISASI MOJA HEWANI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA
YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA MTAA
WA MIANZINI, KATA YA BWAWANI, TARAFA YA KIPEMBAWE, KATIKA MJI MDOGO WA
MAKONGOLOSI, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MHANGA
BAADA YA KUYAONA MAJAMBAZI HAYO ALIPIGA KELELE NA KUPATA MSAADA KUTOKA KWA MAJIRANI HALI ILIYOPELEKEA MAJAMBAZI HAYO KUTUPA
SILAHA NA KUTOKOMEA KWENYE SHAMBA LA MAHINDI.
BAADA YA KUIPATA
BUNDUKI HIYO NA KUIKAGUA ILIKUTWA IKIWA IMEKATWA MTUTU NA KITAKO. AIDHA ENEO LA
TUKIO LIMEOKOTWA GANDA MOJA LA RISASI. UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILO UNAENDELEA
IKIWA NI PAMOJA NA MSAKO MKALI WA KUYATAFUTA MAJAMBAZI HAYO.
KATIKA TUKIO LA PILI
WALINZI @
MABAUNSA WAWILI WA CITY PUB ILIYOPO JIJINI MBEYA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. GOODLUCK KAGALI (23) MKAZI WA ILOMBA NA 2.
MAHAMUD MUINGA (25) MKAZI WA
ILOMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUMSHAMBULIA KWA
KUMPIGA NGUMI NA MATEKE NA KISHA KUMPIGA NA KITU KIZITO MGUU WA KULIA
MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAHATI SANDE (32) MKAZI
WA ISANGA NA KUSABABISHA MGUU HUO KUVUNJIKA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO
MAJIRA YA SAA 01.00 HUKO KATIKA CITY
PUB, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO
CHA TUKIO HILO NI MZOZO ULIOTOKEA BAINA YAO NA MFANYABIASHARA HUYO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA
NA MHANGA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAMKE MMOJA
AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA CHOONI MTOTO MCHANGA MWENYE UMRI WA SIKU MARA
BAADA YA KUJIFUNGUA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015
MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO ENEO
LA MLIMARELI, KATA YA UTENGULE –USONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA,
MSAMALIA MWEMA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA JAPHET
SANGA (41) MWALIMU NA MKAZI WA
MLIMARELI ALIGUNDUA KUTUPWA KWA MTOTO HUYO MCHANGA NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA
NJE KATIKA NYUMBA ANAYOISHI YEYE NA WAPANGAJI WENZAKE BAADA YA KUSIKIA SAUTI YA
MTOTO HUYO AKILIA.
MTOTO HUYO
MWENYE JINSI YA KIKE AMEOKOLEWA AKIWA HAI KWA USHIRIKIANO KATI YA JESHI LA
POLISI NA WANANCHI NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI KWA
MATIBABU/UCHUNGUZI ZAIDI. UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA
KUMTAFUTA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI
KUACHA TABIA YA KUTUPA WATOTO KWANI NI KITENDO CHA KINYAMA, KINYUME CHA MAADILI
NA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHINI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI [MAMA WA MTOTO HUYO] AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA NNE:
WATU WANNE
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ZULFUA ABUBAKAR (30) KONDAKTA WA BASI
LA KAMPUNI YA TAQWA NA MKAZI WA DSM 2.
CHRISTOPHER FREDY (28)
MFANYABIASHARA, MKAZI WA MKOMBOZI TUNDUMA 3.
EMANUEL MWASHAMBWA (35) MKAZI WA
MPEMBA NA 4. STEPHEN KALINGA (29) MKAZI WA MPEMBA WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015
MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI WAKIWA
NA MAZIWA AINA YA LACTOGEN DAZANI 24,
SAWA NA KOPO 1,032 YENYE UJAZO WA GRAM 400 KILA MOJA. THAMANI HALISI YA
BIDHAA HIZO NI TSHS 17,000,000/=.
AIDHA BIDHAA
HIZO AMBAZO ZILIKUWA ZIKIINGIZWA NCHINI BILA KULIPIA USHURU KUTOKA NCHINI
AFRIKA KUSINI, KUPITIA NCHINI ZAMBIA KWA NJIA ZA PANYA.
KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE
MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDITHA JOHN (34) AKIWA NA POMBE YA
MOSHI UJAZO WA NUSU LITA .
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO
TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA MTAA MAPELELE, KATA YA
ILEMI, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE
HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NEHEMIA EMANUEL (22) MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AMBAYE ALIKUWA AKIENDESHA
PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.622
BJV AINA YA SANLG AKIWA AMEPAKIA ABIRIA WAWILI KATIKA PIKIPIKI HIYO MMOJA
WA ABIRIA HAO AKIFAHAMIKA KWA JINA LA MAHENGULA
BONIFACE (30) MKAZI WA MSWISWI NA
MWINGINE AMBAYE ALIRUKA NA KUKIMBIA BAADA YA KUWAONA ASKARI WAKIWA NA MENO YA TEMBO VIPANDE SITA [06].
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA
YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA
KIJIJI CHA MAHANGO-MSWISWI, KATA NA TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA
WA MBEYA.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA BAADA YA KUSIMAMISHWA NA KISHA KUPEKULIWA NA NDIPO KATIKA PIKIPIKI
HIYO KULIKUTWA MFUKO WA SANDARUSI AMBAO NDANI YAKE KULIKUWA NA MENO HAYO YA TEMBO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment