Petro Kalao, MBEYA
wazee
waliojimilikisha maeneo ya serikali katika mtaa wa Gombe kusini kata ya Itezi
jijini Mbeya wametakiwa kuyarejeshe maeneo hayo mikononi mwa wananchi hali iliyozua
mgogoro baina yao na wazee hao.
Viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo Ester
Masawe wamesema eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule na zahanati lakini
wameshangazwa kuona eneo hilo likiuzwa na wazee wa mtaa huo wanaojiita machifu,
bila kuwataarifu viongozi wa mtaa wala wananchi kitendo ambacho kimepelekea
mvutano baina ya wazee hao na wananchi.
Kwa upande wao wazee hao ambao hawakutaka sauti
zao kurekodiwa wamesema kuwa eneo hilo ni eneo la kwao kama waasisi wa chama
cha mapinduzi mtaa wa Gombe kusini, ambapo hata hivyo baada ya wananchi
kukubali kwenda kujiridhisha katika eneo hilo, wao waligoma na kutaka wabakie
katika eneo la mkutano.
Nao baadhi ya waliouziwa maeneo hayo na wazee hao
akiwemo Laurence Malongo maarufu kama mwisho wa reli amesema kuwa eneo hilo anamiliki
kihalali kwani alianza kufanya shughuli za kilimo kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment