Elizabeth Nyivambe, MBEYA
Wakati wananchi wakiendelea kujiandaa
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, Mwenyekiti wa chama cha
demokrsaia na maendeleo Chadema mkoani mbeya John Mwambigija amewataka wananchi
kuendelea kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji huo.
Mwambigija amesema hayo march 13 mwaka huu, wakati
akihutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika
katika eneo la maendeleo kata ya Iyunga jijini mbeya.
amewataka
wananchi mkoani mbeya na kwingineko nchini kuhakikisha wanazingatia haki yao ya
msingi kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao wa oktoba mwaka huu.
Nao baadhi ya viongozi wa Cha chama hicho, wamesema
kujiandikisha ni haki ya kila mwananchi na kuwataka wananchi kuchagua viongozi
wazalendo walio na uchungu na nchi yao wenye kutetea maslahi ya umma.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria
mkutano huo wamesema vyama vya siasa havina budi kuendelea kutoa elimu kwa
wananchi, juu ya umuhimu wa kujiandikisha kwani wananchi wengi hawalichukulii
uzito jambo hilo kufuatia viongozi wao kuwasaliti pindi wanapoingia madarakani.
Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa
kufanyika mwezi oktoba mwaka huu,
ambapo elimu bado inaendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura, ili kushiriki uchaguzi huo, sambamba
na kuipigia kura katiba pendekezwa.
Hata hivyo shughuli zote hizo zina tegemea
wananchi wajitokeza kujiandikisha huku pia mfumo unaotumika kuandikisha wa BVR ukikabiliwa
na changamoto lukuki, ambapo mpaka sasa ni mkoa mmoja tu wa Njombe ndiyo ulioanza
kuandikisha.
No comments:
Post a Comment