NGUVU YA HABARI

Friday, March 13, 2015

WAGANGA WA JADI MBEYA WAONJA JOTO LA POLISI



Jeshi la polisi mkoa wa mbeya limewakamata waganga wa kienyeji 13 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya upigaji ramli chonganishi.

Akito taarifa hiyo kwa vyombo vya habari march 13 mwaka huu, Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmend Msangi amesema waganga hao wamekamatwa kufuatia misako mbalimbali iliofanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa mbeya.

Msangi amesema katika msako uliofanyika wilayani Chunya waganga watano wamekamatwa ambao ni  Hamidu Miraji miaka 41, Doris Elia (42) Chande Simon (43) Aron Mwasinini (70) wote wakazi wa mtanila na Dickson Mwaigaga (37) mkazi wa kibaoni chunya.

Aidha amesema katika msako mwingine walioufanya wilayani Momba, wamekamatwa wapiga ramli wawili ambao ni Noelia Lusambo (40) mkazi wa mkutano,na Edwin Mwambugi (60) mkazi wa chapwa na wilayani Mbozi alikamatwa mganga mmoja aitwaye Abraham Kapelela Simkoko miaka (65) mkazi wa Halungu.

Kamanda Msangi pia amesema katika msako uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la mbeya katika tarafa za sisimba na iyunga, waganga wa jadi na wapiga ramli chonganishi wasiokuwa na vibali walikamatwa ambao ni Maftah seba (51) mkazi wa mwakibete, Gadner mwakasyuka (44) mkazi wa kabwe, Majeshi chawinga (44) mkazi wa ilomba, Msafiri nangale (44) mkazi wa njia panda veta, Mfikemo mwanamaula (50) mkazi wa shewa na Andrew kayange (22) mkazi wa sae.

Kamanda wa polisi mkoa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amesema taratibu za kuwafikisha mahakamani waganga hao zinaendelea.

No comments: