Victor Betram, MBEYA
Mtu mmoja mkazi wa Nsalaga jijini Mbeya
anayeaminika kuwa na Ugonjwa wa akili amemuuwa mtoto mwenye umri wa miaka mitano
kwa kumponda kichwa chake kwa kutumia sululu.
Ambapo mara baada ya tukio hilo wananchi wa eneo
hilo waliamua kujichukulia sheria mkononi na kumteketeza kwa moto mtuhumiwa
aliyefahamika kwa jina la Yona Mwamwile (41) mkazi wa Nsalaga ambaye ni mjomba
wa mtoto huyo.
Mtoto aliyeuawa ametambulika kwa jina la Jonson
Mabanda (5), ambapo akizungumza na kituo hiki Babu wa mtoto huyo ambaye pia ni
baba wa muuaji, amesema kuwa mtoto wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa
akili kwa muda mrefu.
Amefafanua kuwa, mara nyingi hupandwa na kichaa,
na kila anapopandwa na kichaa hushambulia watu na asubuhi ya leo aligundua kuwa
mwanae alikuwa amepandwa na kichaa lakini kabla hawajamdhibiti ndipo
akatekeleza tukio hilo la mauaji.
Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo
alipotafutwa na kituo hiko ili kuelezea tukio hilo, hakuweza kuzungumza
chochote kutokana na uchungu wa kumpoteza mtoto wake.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, wakizunguma na
kituo hiki wamesema walimuona ndugu Mwamwile akimkimbiza mtoto huyo lakini
hawakudhani kama alikuwa na nia mbaya.
Wameeleza kuwa baadaye walisikia kelele kutoka kwa
baadhi ya mafundi waliokuwa wakijenga nyumba ambamo mauaji hayo yametokea na
waliposogea eneo la tukio walimkuta mtuhumiwa akiwa ameshika sululu ambayo
alitumia kumuuwa mtoto huyo.
Wameongeza kuwa, baada ya taarifa hizo kusambaa
wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kuanza kumshambulia mtuhumiwa kwa mawe
na baadaye walimchoma moto na kupelekea kifo chake.
No comments:
Post a Comment