Mtoto
mchanga mwenye umri wa siku moja amekutwa ametupwa katika shimo la choo na mama
yake mzazi katika kijiji cha mlima reli wilayani Mbeya vijijini.
Akizungumza
na Vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi
mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amesema Mwanamke huyo ambaye bado
hajafahamika jina wala makazi yake, amefanya unyama huo siku moja tu mara baada
ya kujifungua motto huyo.
Amesema
tukio hilo limetokea march 13 mwaka huu, majira ya saa nne na nusu usiku eneo la mlimareli, katika kata ya utengule
–usongwe, wilaya ya mbeya vijijini.
Imeelezwa
kuwa aliyegundua kutupwa kwa mtoto huyo mwenye jinsia ya kike ni mwalimu japhet
sanga ambaye pia ni mkazi wa mlimareli baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo
akilia ndani ya shimo la choo cha nje katika nyumba anayoishi yeye na wapangaji
wenzake.
Hata
hivyo Mtoto huyo ameokolewa na jeshi la polisi kwa ushirikiano na wananchi wa
eneo hilo, akiwa hai na amelazwa katika hospitali teule ya ifisi kwa matibabu na uchunguzi zaidi.
Kamanda
Msangi amesemajeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi ikiwa ni pamoja na
kumtafuta mtuhumiwa wa tukio hilo.
Aidha
katika tukio lingine kamanda Msangi amesema kuwa jeshi la polisi linawashikilia
watu wawili waliofahamika kwa majina ya Nehemia
emanuel (22) mkazi wa kijiji cha matundasi na mahengula boniface (30) mkazi wa mswiswi wakiwa na meno ya tembo vipande sita [06].
Watuhumiwa
walikamatwa march 13 katika kijiji
cha mahango-mswiswi wilaya ya mbarali, baada
ya kusimamishwa na kisha kupekuliwa ambapo katika pikipiki yao walikutwa na
mfuko wa sandarusi ambao ulikuwa na meno hayo.
No comments:
Post a Comment