Na Josea Sinkala, Mbeya
Wakati viongozi na wakuu wa mikoa nchini wakitekeleza
agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi wa mazingira disemba 9 mwaka huu,
serikali ya halmashauri ya wilaya ya Mbeya inakabiliwa na changamoto ya kukosa
vifaa vya kufanyia usafi katika mitaro ya maji machafu.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Upendo
Sanga ndiye alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
ofisi ya halmashauri hiyo.
Sanga alisema licha ya kushirikiana na viongozi
mbalimbali na wananchi kwa ujumla kufanya usafi wa mazingira jambo linaloikwamisha
serikali ya halamashauri hiyo kutekeleza agizo la rais kwa kiwango kikubwa ni
kukosa vifaa vya kufanyia usafi hali inayochangia kusababisha mafuriko kipindi
cha mvua na kudai kuwa serikali bado inaendelea kushughulikia.
Pia alisema serikali imewaandikia barua wananchi
waliojenga pembezoni mwa mikondo ya kupitisha maji ili kufanikisha zoezi la
uzibuaji mitalo hiyo.
Alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuzingatia
taratibu za usafi na kusafisha mazingira yao na maeneo ya biashara huku
akiwataka kujitokeza kwa wingi siku ya kilele cha kufanya usafi.
No comments:
Post a Comment