Mbeya, Mwandishi wetu
Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu
uliopita wametakiwa kufanyakazi kwa ushirikiano badala ya kuendeleza itikadi
zao za kisiasa ili kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la mbeya
Vijijini Oran Manase Njeza wakati akizungumza baada ya kumalizika kwa zoezi la
kuwaapisha madiwani wa halmashauri ya mbeya vijijini lililofanyika katika
ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya mbeya.
Mbunge huyo alisema changamoto zinazolikabili
jimbo hilo zinaweza kutatulika endapo viongozi wake wakishikamana na wananchi
wao katika kufanya shughuli za kimaendeleo ambapo amesema shabaha kubwa ya
wananchi wengi ni kuboreshewa sekta ya kilimo kama njia mojawapo ya kujikwamua
kiuchumi.
Aidha Njeza alisema kuwa viongozi hao wana wajibu mkubwa
wa kuwasaidia wananchi kujiajiri badala ya kutegemea ajira serikalini pekee na
kuwakumbusha kuwa wana deni kwa wapiga kura wao kama walivyokuwa wakijinasibu
katika majukwa ya kisisa wakati wa kampeni.
Nao baadhi ya madiwani walioapishwa wakiwemo
waliokuwa wagombea uwenyekiti wa halmashauri wameahidi kushirikiana na viongozi
wengine pamoja na wananchi ili kuleta maendeleo jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment