Kamati Kuu ya CCM Taifa imeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa ilani ya Chama.
Abdulrahman Kinana ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM amesema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.
Kinana alisema kuwa Kamati Kuu kwa niaba ya Chama imeunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali za kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali kwa kuhakikisha kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zinasimamia ukusanyaji wa kodi za Serikali ipasavyo.
Aidha alisema juhudi za serikali ya Awamu ya Tano kwa muda mfupi zimezaa matunda yanayoonekana wazi likiwemo suala la kudhibiti matumizi ya Serikali.
Hata hivyo Kamati Kuu iliwataka wanaCCM na wananchi wote kwa ujumla kumuunga mkono Rais na Serikali yake kwa kuitikia wito wa kufanya kazi kwa bidii, kwa maarifa na uzalendo ili taifa lifikie uchumi wa kati.
No comments:
Post a Comment