NGUVU YA HABARI

Monday, March 16, 2015

Mtoto wa miaka mitano Auawa Kinyama na Muuaji naye Auawa



Victor Betram, MBEYA

Mtu mmoja mkazi wa Nsalaga jijini Mbeya anayeaminika kuwa na Ugonjwa wa akili amemuuwa mtoto mwenye umri wa miaka mitano kwa kumponda kichwa chake kwa kutumia sululu.

Ambapo mara baada ya tukio hilo wananchi wa eneo hilo waliamua kujichukulia sheria mkononi na kumteketeza kwa moto mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Yona Mwamwile (41) mkazi wa Nsalaga ambaye ni mjomba wa mtoto huyo.

Mtoto aliyeuawa ametambulika kwa jina la Jonson Mabanda (5), ambapo akizungumza na kituo hiki Babu wa mtoto huyo ambaye pia ni baba wa muuaji, amesema kuwa mtoto wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili kwa muda mrefu.
Amefafanua kuwa, mara nyingi hupandwa na kichaa, na kila anapopandwa na kichaa hushambulia watu na asubuhi ya leo aligundua kuwa mwanae alikuwa amepandwa na kichaa lakini kabla hawajamdhibiti ndipo akatekeleza tukio hilo la mauaji.


Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo alipotafutwa na kituo hiko ili kuelezea tukio hilo, hakuweza kuzungumza chochote kutokana na uchungu wa kumpoteza mtoto wake.


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, wakizunguma na kituo hiki wamesema walimuona ndugu Mwamwile akimkimbiza mtoto huyo lakini hawakudhani kama alikuwa na nia mbaya.

Wameeleza kuwa baadaye walisikia kelele kutoka kwa baadhi ya mafundi waliokuwa wakijenga nyumba ambamo mauaji hayo yametokea na waliposogea eneo la tukio walimkuta mtuhumiwa akiwa ameshika sululu ambayo alitumia kumuuwa mtoto huyo.

Wameongeza kuwa, baada ya taarifa hizo kusambaa wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kuanza kumshambulia mtuhumiwa kwa mawe na baadaye walimchoma moto na kupelekea kifo chake.




Saturday, March 14, 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14.03.2015.





JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.





RPC.                                                                                         Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                       Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                    
Namba ya simu 2502572                                                                                  S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                           MBEYA.
E-mail:-  rpc.mbeya@tpf.go.tz                                                                      
   tanpol.mbeya@gmail.com


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14.03.2015.


·         WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAJARIBU KUFANYA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWA MFANYABIASHARA WA MADINI AINA YA DHAHABU WILAYANI CHUNYA.


·         WALINZI WAWILI WA CITY PUB JIJINI MBEYA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA NA KUMJERUHI MFANYABIASHARA MMOJA MKAZI WA ISANGA.



·         MWANAMKE MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA MTOTO CHOONI MWENYE UMRI WA SIKU MOJA.



·         WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.



·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI NUSU LITA.



·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAKIWA NA VIPANDE SITA VYA MENO YA TEMBO.







KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA AITWAE ROBERT MBUKWA (50) MFANYABIASHARA YA MADINI AINA YA DHAHABU NA MKAZI WA MIANZINI WILAYANI CHUNYA ALIVAMIWA NA VIJANA WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA SHOT GUN 12 BORE YENYE NAMBA 64943 ILIYOTENGENEZWA KATIKA KIWANDA CHA WEMBLEY @ SCOTT LTD KILICHOPO BIRMINGHAM ENGLAND NA KUFYATUA RISASI MOJA HEWANI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA MTAA WA MIANZINI, KATA YA BWAWANI, TARAFA YA KIPEMBAWE, KATIKA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, MHANGA BAADA YA KUYAONA MAJAMBAZI HAYO ALIPIGA KELELE NA KUPATA MSAADA KUTOKA KWA  MAJIRANI HALI ILIYOPELEKEA MAJAMBAZI HAYO KUTUPA SILAHA NA KUTOKOMEA KWENYE SHAMBA LA MAHINDI.

BAADA YA KUIPATA BUNDUKI HIYO NA KUIKAGUA ILIKUTWA IKIWA IMEKATWA MTUTU NA KITAKO. AIDHA ENEO LA TUKIO LIMEOKOTWA GANDA MOJA LA RISASI. UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILO UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA MSAKO MKALI WA KUYATAFUTA MAJAMBAZI HAYO.


KATIKA TUKIO LA PILI

WALINZI @ MABAUNSA WAWILI WA CITY PUB ILIYOPO JIJINI MBEYA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. GOODLUCK KAGALI (23) MKAZI WA ILOMBA NA 2. MAHAMUD MUINGA (25) MKAZI WA ILOMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA NGUMI NA MATEKE NA KISHA KUMPIGA NA KITU KIZITO MGUU WA KULIA MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAHATI SANDE (32) MKAZI WA ISANGA NA KUSABABISHA MGUU HUO KUVUNJIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01.00 HUKO KATIKA CITY PUB, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI MZOZO ULIOTOKEA BAINA YAO NA MFANYABIASHARA HUYO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA MHANGA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.











KATIKA TUKIO LA TATU:

MWANAMKE MMOJA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA CHOONI MTOTO MCHANGA MWENYE UMRI WA SIKU MARA BAADA YA KUJIFUNGUA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO ENEO LA MLIMARELI, KATA YA UTENGULE –USONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, MSAMALIA MWEMA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA JAPHET SANGA (41) MWALIMU NA MKAZI WA MLIMARELI ALIGUNDUA KUTUPWA KWA MTOTO HUYO MCHANGA NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA NJE KATIKA NYUMBA ANAYOISHI YEYE NA WAPANGAJI WENZAKE BAADA YA KUSIKIA SAUTI YA MTOTO HUYO AKILIA.

MTOTO HUYO MWENYE JINSI YA KIKE AMEOKOLEWA AKIWA HAI KWA USHIRIKIANO KATI YA JESHI LA POLISI NA WANANCHI NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI KWA MATIBABU/UCHUNGUZI ZAIDI. UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI KUACHA TABIA YA KUTUPA WATOTO KWANI NI KITENDO CHA KINYAMA, KINYUME CHA MAADILI NA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHINI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI [MAMA WA MTOTO HUYO] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.


KATIKA TUKIO LA NNE:

WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ZULFUA ABUBAKAR (30) KONDAKTA WA BASI LA KAMPUNI YA TAQWA NA MKAZI WA DSM 2. CHRISTOPHER FREDY (28) MFANYABIASHARA, MKAZI WA MKOMBOZI TUNDUMA 3. EMANUEL MWASHAMBWA (35) MKAZI WA MPEMBA NA 4. STEPHEN KALINGA (29) MKAZI WA MPEMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI WAKIWA NA MAZIWA AINA YA LACTOGEN DAZANI 24, SAWA NA KOPO 1,032 YENYE UJAZO WA GRAM 400 KILA MOJA. THAMANI HALISI YA BIDHAA HIZO NI TSHS 17,000,000/=.

AIDHA BIDHAA HIZO AMBAZO ZILIKUWA ZIKIINGIZWA NCHINI BILA KULIPIA USHURU KUTOKA NCHINI AFRIKA KUSINI, KUPITIA NCHINI ZAMBIA KWA NJIA ZA PANYA.





KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDITHA JOHN (34) AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA NUSU LITA .

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA MTAA MAPELELE, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.


KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NEHEMIA EMANUEL (22) MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AMBAYE ALIKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.622 BJV AINA YA SANLG AKIWA AMEPAKIA ABIRIA WAWILI KATIKA PIKIPIKI HIYO MMOJA WA ABIRIA HAO AKIFAHAMIKA KWA JINA LA MAHENGULA BONIFACE (30) MKAZI WA MSWISWI NA MWINGINE AMBAYE ALIRUKA NA KUKIMBIA BAADA YA KUWAONA ASKARI WAKIWA NA MENO YA TEMBO VIPANDE SITA [06].

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHANGO-MSWISWI, KATA NA TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA BAADA YA KUSIMAMISHWA NA KISHA KUPEKULIWA NA NDIPO KATIKA PIKIPIKI HIYO KULIKUTWA MFUKO WA SANDARUSI AMBAO NDANI YAKE KULIKUWA NA MENO HAYO YA TEMBO.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


 

Mgogoro wa ardhi Wawakumba wazee wa Itezi, Mbeya



Petro Kalao, MBEYA

wazee waliojimilikisha maeneo ya serikali katika mtaa wa Gombe kusini kata ya Itezi jijini Mbeya wametakiwa kuyarejeshe maeneo hayo mikononi mwa wananchi hali iliyozua mgogoro baina yao na wazee hao.

Viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo Ester Masawe wamesema eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule na zahanati lakini wameshangazwa kuona eneo hilo likiuzwa na wazee wa mtaa huo wanaojiita machifu, bila kuwataarifu viongozi wa mtaa wala wananchi kitendo ambacho kimepelekea mvutano baina ya wazee hao na wananchi.

Kwa upande wao wazee hao ambao hawakutaka sauti zao kurekodiwa wamesema kuwa eneo hilo ni eneo la kwao kama waasisi wa chama cha mapinduzi mtaa wa Gombe kusini, ambapo hata hivyo baada ya wananchi kukubali kwenda kujiridhisha katika eneo hilo, wao waligoma na kutaka wabakie katika eneo la mkutano.

Nao baadhi ya waliouziwa maeneo hayo na wazee hao akiwemo Laurence Malongo maarufu kama mwisho wa reli amesema kuwa eneo hilo anamiliki kihalali kwani alianza kufanya shughuli za kilimo kwa muda mrefu.


Kichanga cha tupwa Chooni



Mtoto mchanga mwenye umri wa siku moja amekutwa ametupwa katika shimo la choo na mama yake mzazi katika kijiji cha mlima reli wilayani Mbeya vijijini.

Akizungumza na Vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amesema Mwanamke huyo ambaye bado hajafahamika jina wala makazi yake, amefanya unyama huo siku moja tu mara baada ya kujifungua motto huyo.

Amesema tukio hilo limetokea march 13 mwaka huu, majira ya saa nne na nusu usiku eneo la mlimareli, katika kata ya utengule –usongwe, wilaya ya mbeya vijijini.

Imeelezwa kuwa aliyegundua kutupwa kwa mtoto huyo mwenye jinsia ya kike ni mwalimu japhet sanga ambaye pia ni mkazi wa mlimareli baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia ndani ya shimo la choo cha nje katika nyumba anayoishi yeye na wapangaji wenzake.

Hata hivyo Mtoto huyo ameokolewa na jeshi la polisi kwa ushirikiano na wananchi wa eneo hilo, akiwa hai na amelazwa katika hospitali teule ya ifisi kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Kamanda Msangi amesemajeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa wa tukio hilo.

Aidha katika tukio lingine kamanda Msangi amesema kuwa jeshi la polisi linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya Nehemia emanuel (22) mkazi wa kijiji cha matundasi na mahengula boniface (30) mkazi wa mswiswi wakiwa na meno ya tembo vipande sita [06].

Watuhumiwa walikamatwa march 13 katika kijiji cha mahango-mswiswi  wilaya ya mbarali, baada ya kusimamishwa na kisha kupekuliwa ambapo katika pikipiki yao walikutwa na mfuko wa sandarusi ambao ulikuwa na meno hayo.