NGUVU YA HABARI

Sunday, March 9, 2014

IMANI ZA KISHIRIKINA ZAHAMISHIA IBADA CHOONI JIJINI MBEYA, WACHUNGAJI NA WAUMINI WA PENTEKOSTE WAUNGANA NA KUWEKA KAMBI CHOONI



Waumini wa kanisa la Pentekoste Holiness Association Mission in Tanzania pamoja na wachungaji wa makanisa jirani na kijiji cha Iyunga Mapinduzi, wilaya ya Mbeya vijiji, jijini Mbeya wamefanyia ibada ibada katika eneo la choo baada ya mshirika wa kanisa hilo kuingia katika choo hicho na kukuta kimejaa nguo, madumu na chupa zenye damu pamoja na nyama zinazosadikiwa kuwa za binadamu na wanyama.
Kwa mjibu wa shuhuda watukio hilo la namna yake Eliza Subiri  amesema aliingia katika choo hicho kwa lengo la kujisaidia ndipo akaiona chupa katika shimo la choo, jambo lililomsababisha aende kwa mchungaji wa kanisa hilo na kumwambia kile achokiona.
Kama maigizo vile, baada ya mchungaji kuingia katika choo hicho akashuhudia mengi zaidi ya vile alivyoviona muumini huyo. Mchungaji na shuhuda wa tukio hilo waliamu akuripoti tukio hilo kwa majirani na serikali ya kijiji hicho.


Tukio hilo la namna yake limewaunganisha wachungaji na waumini wa makanisa zaidi ya matano na kufanya Ibada ya pamoja kwa ajili ya maombezi katika eneo hilo.
Kwa upande wao wachungaji waliofanya mahojiano na blogu hii wanazungumziaje tukio hilo? 
Bofya hapa uwasikilize....
wachungaji na waumini kwa pamoja leo walikubaliana kuchoma moto vitu hivyo, lakini serikali ya kijiji hicho imewazuia wasichome moto leo na hivyo kuwataka kesho wachome mto vitu hivyo kwa kushirikiana na serikali ya kijiji hicho.

Nao mashuhuda walioshuhudia maajabu hayo wametoa ushuhuda wao na kuwaasa watanzania kumtegemea Mungu kwa moyo wote na kwa kila jambo kwa kuwa siku za mwisho zimekaribia.

Moja ya mashuhuda hao Lone Mkono amesema matukio kama hayo yanaashiria mwisho wa dunia na kuwataka wakristo wasife moyo kwa sababu ya majaribu wanayo yapata.
Kwa mjibu wa mchungaji mwenyeji wa kanisa hilo amesema mara nyingi kanisa hilo tangu lijengwe limekuwa likiangukaanguka kuta zake mara kwa mara, hivyo na tukio hilo ameliunganisha na matukio mengine yanayolikabili kanisa hilo kuwa ni mipango ya shetani kutaka kulirudisha nyuma kanisa hilo.
Bofya hapa kupata sauti za mashuhuda wachungaji na mchungaji mwenyeji kasema nini

No comments: