NGUVU YA HABARI

Tuesday, December 24, 2013

CHRISMASI NI MWANZO WA UKOMBOZI WA MWANADAMU

Wakristo nchini Tanzania wametakiwa kusherehekea Sikukuu ya  kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kuwasaidia wasiojiweza kuashiria kuwa wanatambua maana ya Krismasi na umuhimu wake kama Mungu alivyomtoa mwanae Yesu Kristo kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu mikononi mwa shetani.
Mchungaji wa Kanisa la Elimu Pentekoste lililopo Airport jijini Mbeya,  Jerome Steven Saninga akihojiwa na mwandishi wa blogu hii na radio Mlimani alisema wakristo wanatakiwa kuzingatia umuhimu wa kuzaliwa kwa Yesu kristo na kutenda matendo yaipasayo injili ambayo Mungu aliwatendea wanadamu kwa kumtoa Mwana wake wa peke Yesu Kristo azaliwe duniani kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu.
Mchungaji Saninga alisema wakristo wanatakiwa kuadhimisha Krismasi kwa kupinga na kulani vitendo vyote vilivyo kinyume na mpango wa Mungu kama vile mauaji, ubakaji, ulevi kwa kuhubiri Injili ya Yesu Kristo kwa imani na matendo.

Naye Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia ni Mbuge wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA) alipohojiwa kwa njia ya Simu alisema ni wakati mzuri kwa Watanzania na wakristo kwa ujumla wakatumia kipindi hiki cha Krismas kuwasaidia watoto yatima, wajane na wagonjwa waliopo hospitalini na majumbani baadala ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa mambo ya anasa kama vile kulewa.

“Tunasherehekea Krismasi hii lakini kila mtu kwa mmoja mmoja atafakari Kwamba hakuja duniani kwa bahati mbaya na aone ni aibu kwa kufa na anazikwa bila mchango wa maana kwa jamii.
“Ni wakati mwafaka wa kuonesha upendo wako kwa watu badala ya kufanya mambo ambayo ni kinyume kabisa na maneno ya Mungu na pia kuonesha upendo kwa jamii inayotuzunguka kama vile kutembelea yatima na wagonjwa wapo hospitalini,”
Kupata sauti ya Mchungaji Msigwa bofya hapa............https://soundcloud.com/user442431332/mchungaji-msigwa-ahimiza
Nini Maana ya Krismasi?
“Krismasi ni kati ya Sikukuu mojawapo ambazo huadhimishwa na Wakristo ulimwenguni kote wakikumbuka siku ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo  ambaye alizaliwa ili kumkomboa mwanadamu mikononi mwa adui shetani  aliyekuwa akiwatawala wanadamu na kuwatenga wanadamu hao  na Mungu wao kwa sababu ya dhambi wazitendazo,” Mchungaji saninga alitoa maana ya krismas.
Mchungaji Saninga akiombea maji wakati wa kubatiza waongofu wapya mkoani Mbeya

Aidha, Mchungaji Saninga aliwaasa wakristo kuonesha upendo wa dhati katika kipindi hiki cha Krismasi kwa kuwa wanaadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mwokozi wa wanadamu na kuachana na mambo ya anasa kipindi hiki cha Sikukuu.
Kupata Sauti ya Mchungaji Saninga Bofya hapa............................https://soundcloud.com/user442431332/mchungaji-saninga-mahojiano
Naye Mchungaji Peter Msigwa alisema Krismasi ni siku ambayo baadhi ya Wakristo huadhimisha Kila ifikapo tarehe 25 mwezi Disemba kama ishara ya kukumbuka miaka 2000 iliyopita ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambayo ni Mkombozi wa ulimwengu baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika Bustani ya Edeni na kutengana na Mungu.
“Krismas ni mwanzo wa ukombozi wa mwanadamu ambao hukamilishwa na ufufuo wa Yesu Kristo”.
Je, ni kweli Yesu Kristo alizaliwa tarehe 25 mwezi wa 12?
Akijibu swali hilo Mchungaji Saninga alisema si kweli kuwa Yesu alizaliwa tarehe 25 mwezi wa 12 bali ni tarehe ambayo wanathiologia walikaa na kukubaliana iwe siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo kama ishara ya kutambua umuhimu wa kuzaliwa kwake.
Aliongezakuwa waafrika wanasherekea Sikukuu hii kwa kufuata Kalenda za Wayahudi ambayo alidai wana kalenda mbili, kalenda ya Kidini na kalenda ya kiserikali tofauti na waafrika ambao wanatumia kalenda moja waliyoridhishwa na wakoloni.
“Ni vema mkristo au mtu ye yote akaruhusu Yesu kristo azaliwe ndani ya moyo wake, na hili ni jambo linalotakiwa kufanyika kama ilivyoandikwa katika Ufunuo 3:20; Tazama, nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu ye yote akisikia sauti Yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye,naye pamoja name,” alisema mchungaji Saninga.
 Hata hivyo mchungaji Saninga amewataka Wakristo kusherekea sikukuu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Krismas) kwa kuangalia umuhimu wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambaye alikuwa kufanya suluhu la ukombozi wa mwanadamu baada ya mwanadamu kujitenga na Mungu kwa sababu ya dhambi.
Krismasi ni sikukuu ambapo Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe6 Januari katika ule wa mashariki
                       
Hata hivyo kwa mjibu wa http://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi#Historia_ya_Krismasi inaonesha kuwa hakuna tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo kutokana na kutojulikana utamaduni wa Wayahudi kuhusiana na kukumbuka siku ya kuzaliwa kwake.
Hata hivyo vitabu vya historia ya Kristo vinaonesha kuwa Sikukuu ya Krismasi ilianzishwa na nchi ya Roma na mataifa ya kati ambayo yalikuwa na hamu ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi wao na baadaye mataifa mengine yakaunga mkono.
Habari nyingine zinadai kuwa Krismasi ilikadriwa na wataalamu wa nchi ya Misri ambao walidai kuwa kikundi cha wakristo wa Basilides wa Misri waliosherehekea siku ya kuzaliwa Kristo tarehe 6 Januari kila mwaka na wengine wakikadria tarehe 25 mwezi Desemba.

Sunday, December 22, 2013

FILIPO PHIRI: Nguo fupi, matiti nje, milegezo marufuku walokole

A
skofu msaidizi wa Jimbo la Kinondoni na Mchungaji  wa kanisa la EAGT Mikocheni ‘A’ Filipo Phiri apiga marufuku kwa waumini wote uvaaji wa nguo fupi, mlegezo na unyanyuaji matiti kwa wanawake na mavazi yasiyoendana na misingi ya dini pamoja  na utamaduni wa Mwafrika, asema yarudisha nyumba Injili ya Kristo.
Akihutubia waumini wa kanisa hilo lililopo Samaria Mikocheni A Desemba 22 mwaka huu, mchungaji Phiri alisema wakristo wanaovaa nguo fupi hawana nia ya kukuza injili kwa mataifa zaidi ya kuwaingiza majaribuni waumini wenzao na hata mataifa wanaotaka kuwahubiria na hivyo kuwa kikwazo katika kueneza injili ya Yesu Kristo kwa Mataifa.
Aliongeza kuwa wanawake wanatakiwa kuvaa nguo fupi (nusu uchi) wakati wakiwa na wanaume zao  katika maandalizi ya tendo la ndoa na si kuvaa nguo fupi kanisani kila mahali kwa kuwa huhizi heshima zao.
Pia, mchungaji Phiri alikemea tabia ya wanawake kunyanyua matiti yaonekane juu kwa madai kuwa (wasichana) wengi hawataki yaonekane matiti yao yameanguka (yamelala) jambo ambalo mchungaji alidai limekuwa likiwaingiza vijana majaribuni kwa kuwatamani wasichana hao pindi wakiyaangalia matiti (maziwa) ya wanawake hao.
“Tabia ya kuacha maziwa yenu yaonekane kwa watu, na kunyanyua maziwa yenu kwa kuvaa kanchiri (sidiria) ndogo si desturi yetu walokole wala Waafrika bali mmeiga tu.
“Nikimwona mwanamke amevaa nusu uchu au nguo vupi, amenyanyua maziwa kuwatega vijana wangu nitamfukuza mbele ya kanisa hata kama yupo kutoa sadaka madhabahuni,” alisisitiza mchungaji Phiri.
Aidha Mchungaji Phiri aliwataka vijana wanaovaa suruali mlegezo maarufu kata ‘K’ kuacha tabia hiyo mara moja vinginevyo nao atawafukuza kanisa akidai kuwa nao wanazui in jili ya Yesu Kristo isisonge mbele kwa kuwa mlegezo huvaliwa na watu wasiokoka na waliokosa heshima mbele za watu.
“Nikikuona umevaa mlegezo makalio yako yanaoneka ama chupi yako inaonekana, I cannot tolerate you, I chase you out (siwezi kukuvumilia, nitakifukuza),” mchungaji Phiri aliwasisitizia vijana waliookoka.
Hata hivyo, mchungaji Phiri aliwataka wanaume kukaa na wake zao na kuwaonya juu ya mavazi wanayovaa mbele za watu na kuwaambia kuwa wajue kuwa mwanamke anatakiwa kuonesha mapaja, maziwa yake kwa mwanamume wake tu, na kwa watu wengine mwanamke anatakiwa kusetiri mwili wake kwa mavazi.
Vivyo hivyo, kwa wanaume aliwatakiwa kutoacha vifua wazi, kuvaa kaptura akidai kuwa si tabia ya watu waliookoka kuvaa mavazi yayowavunjia heshima mbele za watu.
Hayo yote aliongea wakati akifundisha somo la MSIMAMO WA WOKOVU akisoma Mathayo 7: 24-27, Yuda 1:3-5 na 1Wakorintho 2:4-8
Bofya link hii ukitaka sauti
https://soundcloud.com/user442431332/filipo-phiri-nguo-fupi-matiti